Monday, December 8, 2014
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AFANYA TENA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA
Do you like this story?
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmoja wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya
kaziwengine sita kuanzia jana, Jumamosi, Desemba 6, 2014.
Taarifa iliyotolewa Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu
Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais
amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix Ntibenda
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Ndugu Ntibenda ataapishwa leo, Jumatatu, Desemba 8, 2014,
saa nne asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.
Taarifa hiyo inasema kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi
ni Mheshimiwa Elaston Mbwilo anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa
wa Simiyu ambako anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa likizo
ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa Manyara kutoka
Mkoa wa Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa
Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.
Wengine ni Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa
Mkoa wa Tanga kutoka Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza
anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa Mhandisi
Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka Mkoa wa Arusha.
Wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao
vya sasa vya kazi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Desemba,2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AFANYA TENA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA”
Post a Comment