Thursday, December 18, 2014

MSWAADA TATA WAZUA VURUGU BUNGENI KENYA




Wabunge wa Kenya wametofautiana pakubwa bungeni kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabnunge w aupinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.

Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.

Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.'

Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.

Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
Via>BBC

0 Responses to “MSWAADA TATA WAZUA VURUGU BUNGENI KENYA”

Post a Comment

More to Read