Thursday, December 18, 2014

TIBAIJUKA AGOMA KUJIUZULU





NA CHALILA KIBUDA WA MICHUZI BLOG
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka amesema kuwa hawezi kujiuzulu katika nafasi  ya uwaziri kutokana fedha ya Tegeta ESCROW.

Akizungumza  na Waandishi na Habari mapema leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Hayyat Regency,Anna alisema kuwa udalali wake fedha hiyo ni kwa ajili ya wanafunzi katika shule  za Taasisi ya  Johansson  Girls Education Trust.
Alisema fedha hiyo aliyoipata ni ni bil 1.66 ambazo zilitoka katika kampuni ya James Rugemalira ni kwa ajili ya msaada wa shule  za Taasisi ya  Johansson  Girls Education Trust .

Alisema kuwa fedha hiyo kuingia katika akauti yake binafsi ilitokana na masharti ya mtoa msaada ndugu James  Rugemalira  ambaye alitaka fedha hiyo iingie katika akauti ya Benki ya Mkombozi. ‘’Nikijiuzulu hata Rais Jakaya Kikwete atanishangaa kwani fedha nilizopata ni za shule na kwa ajili kukomboa elimu nchini  hasa kwa watoto wa kike kutokana na wazazi wengi kutoweza kumudu gharama za shule’’alisema Anna.

Alisema kuwa udalali wake ni kutafuta  fedha kwa ajili ya elimu nchini ambapo, alidai hata Mwenyekiti wa Makampuni  ya IPP ,Reginard Mengi alitoa sh.milioni 248 kwa ajili ya msaada wa shule hiyo.

Anna alisema kuwa  wananchi watambue kuwa yeye ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa hivyo hawezi kufanya hivyo na kama angetaka fedha hiyo angeweza kufuata hata katika shule na kuchukua.

0 Responses to “ TIBAIJUKA AGOMA KUJIUZULU ”

Post a Comment

More to Read