Thursday, December 18, 2014

RAIS KIKWETE AMTEUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MPYA BAADA YA JAJI WAREMA




Habari zilizitufikia  hivi punde zinadai kuwa Rais Dr Jakaya  Kikwete amemteua  Prof Ibrahim Juma kuwa mwanasheria mkuu wa  serikali kuziba nafasi  iliyoachwa  wazi na  aliyekuwa   mwanasheria mkuu jaji  Frederick warema  aliyejiuzulu baada  ya  shinikizo la  wabunge  kufuatia  sakata  la Tegeta Escrow

Jaji
P rof. Ibrahim Hamis Juma,Jaji wa Mahakama ya Rufani,hakuwahi
kuiangusha Serikali kwenye maamuzi yake. Tangu akiwa Mahakama Kuu,Jaji
Juma aliilinda kwa nguvu zake zote Serikali ya Chama cha Mapinduzi.
Analipa fadhila kwa rafikiye Rais Jakaya Mrisho Kikwete.


Kiuweledi,Jaji Prof.Juma ni msomi washeria
aliyebobea. Ana uwezo mkubwa sana. Lakini,maisha yanampokonya matumizi
sahihi ya weledi wake. Ndivyo mambo yanavyotakiwa kuwa?!Akiwa Mkuu wa
Kitivo cha Sheria,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Prof.Juma aliwahi
‘kumsave’ Wakili Msomi Ridhiwani Kikwete ambaye ‘alidisco’. Alimsimamia
kidete hadi akabaki nakumaliza masomo yake mwaka 2005 na kutunukiwa
Shahada ya Kwanza ya Sheria.


Jaji Prof. Juma alianza kulipwa alichokifanya kwa
Ridhiwani mwaka 2007 pale alipoteuliwa kweye Tume ya Kuchunguza Mauaji
ya wafanyabiashara watatu maeneo ya Sinza. Tume hiyo iliyoundwa na Rais
iliongozwana Jaji Kipenka Musa.Baadaye,Jaji Prof.Juma aliteuliwa kuwa
Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2008. Akiwa hapo,Shauri la uchaguzi kati ya
Makongoro Mahanga na Fred Mpendazoe likaletwa mbele yake. Kila mtu
anafahamu kilichotokea. Kwa kukumbuka tu,Mahanga aliibuka mshindi na CCM
‘ikapeta’.


Mwishoni mwa mwaka jana,Jaji Prof.Juma
alipandishwa cheo na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Hapo ndipo
lilipomkuta Shauri lililotolewa uamuzi jana:Shauri la Aeshi Hilary dhid
ya NorbertYamsebo.Mlitegemea matokeo tofauti? Ingawa shauri la Yamsebo
lilisikilizwa na jopo la Majaji watatu: Jaji Edward Rutakangwa,Jaji
Stephen Bwana na Jaji Prof.Ibrahim Hamis Juma,bado Jaji Juma alikuwa na
nafasi yake kubwa katika shauri hilo.

Tasnia ya sheria inafanana na ya jeshi.‘Mdogo’
hutumwa na kutumikia zaidi.’Seniority’ ndio kila kitu. Kwa
‘ukubwa’katika jopo hilo,Jaji Rutakangwa anaanza,halafu Jaji Bwana na
tena Jaji Prof.Juma. Hivyo basi,kazi kubwa ilifanywa na Jaji Prof.Juma.
Mwenye kuamini na aamini. Majaji wawili waliobaki wao ‘wali-vet’
kilichoandaliwa na Jaji Prof.Juma.

Sina mashaka na uwezo wa Jaji
Prof.Juma.Ninamashaka na mahusiano yake na mkuu wa Serikali na chama.
Kwa mahusiano hayo,CHADEMA waweza kufurukuta mbele ya Jaji huyu?
Sidhani. CHADEMA watakuwa wanapiga mwereke mbele yake kila shauri.Labda
aamue kutumia weledi wake ipasavyo.

0 Responses to “RAIS KIKWETE AMTEUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MPYA BAADA YA JAJI WAREMA”

Post a Comment

More to Read