Thursday, December 11, 2014

MWANAMKE APANDISHWA KIZIMBANI MBEYA AKIDAIWA MILIONI 1 BAADA YA KUFUMANIWA NA MUME WA MTU




Mwanamke mmoja mkazi wa Majengo jijini Mbeya Rose Samuel mwenye miaka 21 juzi alifikishwa mahakamani akidaiwa fidia ya shilingi milioni 1 kwa tuhuma za kufumaniwa na mume wa Mwanahamisi Omari mwenye miaka54.

Katika kesi hiyo Rose anaiomba mahakama ya mwanzo imuamuru mdaiwa huyo kulipa kiwango hicho cha fedha kutokana na kufumaniwa akiwa na mumewe.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Onesmo Zunda  atasikiliza kesi hiyo leo baada ya washtakiwa kutoa maelezo ya awali.

Katika maeleo yake ya awali Rose alidai kuwa alimfumania mwanamke huyo usiku wa kuamkia Desemba3 nyumbani kwa mwanaume huyo hata hivyo mshtakiwa alikana  shtaka mahakamani hapo na hakimu kuahirisha kesi akidai hataki kupoteza mda mwingi kufikia maamuzi.

0 Responses to “MWANAMKE APANDISHWA KIZIMBANI MBEYA AKIDAIWA MILIONI 1 BAADA YA KUFUMANIWA NA MUME WA MTU ”

Post a Comment

More to Read