Tuesday, December 2, 2014
MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI JOSEPH NYUKI AKAMATWA NA POLISI KISA KUUZA CD HUKU ANAPIGA KELELE MTAANI HUKO IRINGA.
Do you like this story?
Balozi wa Yesu akionyesha CD yake mpya ya Saluti ambayo alikuwa akiiuza mtaani kabla ya kuwapigia saluti polisi waliomkamata kwa muda |
Balozi wa Yesu akienda kupanda gari |
Wananchi Iringa wakiwa wamelizunguka gari la Balozi wa Yesu leo |
Askari polisi akimthibiti balozi wa Yesu |
MWIMBAJI
wa nyimbo za injili maarufu nchini Tanzania ambaye ni
mlemavu wa mkono mmoja Mwinjilisi Joseph Nyuki maarufu kwa
jina la Balozi wa Yesu amejikuta mikononi wa polisi
wakati akiendesha harambee yake ya Injili mtaa kwa Mtaa mjini Iringa.
Tukio
hilo la balozi wa Yesu kukamatwa na polisi
limetokea leo majira ya saa 8 mchana wakati gari la mwimbaji
huyo wa Injili likipita katika mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kueneza
injili kwa kuuza CD inayokwenda kwa jina la Saluti .
Mbali ya
kuwa na kibali cha Manispaa ya Iringa kinachompa
uhuru wa kueneeza injili kwa watu wote kupitia CD hiyo ya
Saluti na kibali hicho kupitishwa polisi bado
askari polisi walimfuata balozi huyo wa Yesu na kumtia
nguvuni kuwa hapaswi kueneza injili kwa kupiga
kelele mitaani.
Askari
ambae jina lake halikuweza kunaswa mara moja
alifika katika gari lenye namba za Usajili T 364 DPD ambalo
lilikuwa limefunga muziki mnene na kupeperusha
injili mtaani kiasi cha kila mmoja mjini hapa kuvutiwa na vionjo
vya mwimbaji huyo na kulifuata gari hilo kununua CD
kabla ya askari huyo kulipiga pini gari hilo eneo
la Soko kuu Miyomboni mjini Iringa .
Baada ya
kumsimamisha mwimbaji huyo kutoendelea na uuzaji wa CD hiyo askari
huyo alimtaka kuonyesha kibali pamoja na kuzima muziki na
kugeuza gari hilo kupeleka Polisi amri ambayo bila
jeuri balozi wa Yesu alitii huku akisema ndio kazi ya
kueneza injili hiyo ambayo kwake ameizoea .
Kwa
upande wao wananchi ambao walikuwa wakinunua CD
wameeleza kusikitishwa na hatua ya polisi kuzuia
uenezaji wa injili huku kila siku mji wa Iringa watu wanapita
na magari wakitangaza Ma Disco na matamasha yenye vichocheo
vya maambukizi ya VVU huku wakiyafumbia macho.
Mtandao
huu ulipofuatilia sakata hilo kituo
cha polisi ulishuhudia suala hilo likiishia nje ya
kituo cha polisi baada ya askari huyo kuyamaliza kiume
na mwimbaji huyo nje ya kituo baada ya kuonyesha kibali halali cha
Manispaa ya Iringa na wakati askari huyo akihoji zaidi juu ya
kuzunguka kila kona likiwemo eneo hilo la polisi kwa
kupiga muziki ghalfa Mungu alionyesha nguvu zake kufuatia
gari jingine lililokuwa likiuza simu huku
likipiga miziki ya duniani likipita nje ya kituo cha polisi
bila kukamatwa ndipo askari kwa kuona hilo walimruhusu
kuendelea na kazi ya kuitangaza injili.
Akizungumza na
mtandao huu mara baada ya kuachiwa huru Balozi wa Yesu
alisema kuwa polisi walifika na kumsimamisha na
kumwomba kibali na baada ya kuonyesha aliachiwa huru na
kuwa polisi wametimiza wajibu wao na kuwa hana kinyongo
nao.
Pia
alisema kuwa ziara yake mkoani Iringa na mikoa mbali mbali ni
kuitangaza injili kupitia oparesheni yake ya Injili mtaa kwa
Mtaa kwa watu wote waokoke na kuwa
anaifanya hivyo kama njia ya kuuza CD yake baada
ya kuchoshwa na unyonyaji unaofanywa na baadhi ya studio kwa
kuwalalia waimbaji wa nyimbo za Injili nchini.
via>>Matukiodaima
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI JOSEPH NYUKI AKAMATWA NA POLISI KISA KUUZA CD HUKU ANAPIGA KELELE MTAANI HUKO IRINGA.”
Post a Comment