Wednesday, December 10, 2014

RC KANDORO ASHUHUDIA TIMU YAKE IKIADHIBIWA NA VIONGOZI WA DINIKATIKA MCHEZO WA AMANI SOKOINE MBEYA


Timu ya Viongozi wa Serikali ya jiji la Mbeya

Timu ya Amani






Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Noumani Sigara akiwatoka wachezajia wa timu ya amani katiaka uwanja wa Sokoine jijini mbeya




Mchungaji akionyesha juu kombe mara baada ya kushinda na kuibuka washindi kwa kuwa charaza tiimu ya viongozi wa serikali goli 4 kwa 2



Tanzania imetimiza miaka 53 ya uhuru katika kusherekea  sikukuu hii ya pekee mkoani mbeya kulikuwa na burudani ya aina yake katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini hapa.

Viongozi wa dini walikutana na viongozi wa serikali  na kusakata kabumbu la aina yake  uku wakishambuliana kwa zamu lakini viongozi wa dini walionekana kuwa imara na kutawala mchezo huo.

Henry Katanga aliwanyanyua mashabiki wa dini baada ya kuifungia timu yake goli la kwanza dakika ya 6 ya mchezo mashambulizi yaliendelea ktika lango la viongozi wa serikali ambapo shehe salum aliweka goli la pili dakika ya 27 waliongeza lingine kupitia kwa lucky Sigalla na kuandika goli tatu.

Pr.Norman Sigalla alipachika goli la kufutia machozi dakika ya 25 kipindi cha kwanza hadi timu hizo zinaenda mapumziko viongozi wa dini walikuwa mbele kwa goli tatu kwa moja dhidi ya viongozi wa serikali.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa kasi kasi hiyo iliweza kusaidia kwa viongozi wa dini na kufanikiwa kuongeza goli la nne  kabla ta King Sigalla kuongeza goli la pili kwa serikali kwa mkwaju wa penart mpaka dakika tisini zinamalizika dini 4 serikali 2.
Akizungumza na fahari news Normani sigalla alisema tumefungwa sababu ya kutofanya mazoezi.

“Hatukuwa na mda wa kufanya mazoezi kwa saabu mda mwingi tulikuwa tunashughulikia ujenzi wa maabara na kzi za kiserikali lakini tunashukuru sababu ni mchezo wa kudumisha amani.”alisema Sigalla
Shekhe Salum naye aliongeza kwa kusema ushindi walioupata ni mazoezi .

”Mazoezi tuliyofanya yamesaidia kufanya vizuri katika mchezo huu wa kudumisha amani ya taifa letu katika kuadhimisha miaka 53 ya uhuru.”

Vikombe vilienda kwa timu za dini kwa upande wa mpira wa miguu na pete baada ya kuibuka washindi uku mchezaji bora Norman sigalla  na mfungaji bora Sekhe salum .

TIMU YA AMANI

0 Responses to “RC KANDORO ASHUHUDIA TIMU YAKE IKIADHIBIWA NA VIONGOZI WA DINIKATIKA MCHEZO WA AMANI SOKOINE MBEYA”

Post a Comment

More to Read