Monday, December 8, 2014
VIONGOZI WA DINI NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MBEYA KUTOANA JASHO KESHO KATIKA UWANJA WA SOKOINE
Do you like this story?
Mkuu wa wa mkoa
wa mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa Madhehebu ya Dini Mkoa wa Mbeya, Askofu wa
kanisa la Anglikana Mkoa wa Mbeya, John Mwela
|
Desember 9, mwaka huu katika kuadhimisha miaka 53 ya uhuru
viongozi wa dini wanatarajia kujitupa katika Uwanja wa Sokoine wa Jiji la
Mbeya na kulisakata kabumbu kwa lengo la kudumisha amani iliyopo nchini.
Mtanange huo
utawajumisha Masheikh,Maimamu,Maaskofu,Wach ungaji, Mapadre na viongozi wote wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya, huku mgeni rasmi atakuwa
mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro.
Akizungumza jijini Mbeya leo, Desember
6,2014, Mwenyekiti wa Madhehebu ya Dini Mkoa wa Mbeya, Askofu wa kanisa la
Anglikana Mkoa wa Mbeya, John Mwela, alisema mwamuzi wa mpambano huomgeni rasmi
ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro.
Amefafanua kuwa viongozi hao wa dini tayari wameshaanza
mazoezi kwa jili ya kujiweka tayari kwa ajili ya kufanya vizuri katika mtangane
huo wa kuhamasisha amani na ulivu nchini.
Amesema, mpaka
sasa kamati ya maandalizi imepokea timu moja ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa Mbeya kushiriki mtanange huo na kwamba bado kamati imetoa nafasi kwa
timu mbalimbali za kijamii kufika kujiandikisha.
Amebainisha kuwa , michezo
itakayochezwa siku hiyo ni mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba,
kukimbiza kuku pamoja kukimbia kwenye magunia hivyo amewataka wananchi
kujitokeza siku hiyo kushuhudia mtanange huo .
Hata hivyo, viongozi wa madhehebu ya dini, wameonyesha
kutotishwa na wapinzania hao kwani wao wamedai kuwa timu yao ipo kamili na
kwamba siku hiyo inatarajia kuibuka na ushindi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VIONGOZI WA DINI NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MBEYA KUTOANA JASHO KESHO KATIKA UWANJA WA SOKOINE”
Post a Comment