fahari News
Habari | Michezo | Bishara | Zabuni
Home
BIASHARA
KITAIFA
KIMATAIFA
USA
AFRIKA
AFRIKA MASHARIKI
MICHEZO
MUZIKI
SIASA
Recommended:
Perfect Social Media Marketing Stratergy For Your Business
Like
Saturday, January 3, 2015
PANYA ROAD WATIKISA JIJI LA DAR
Tweet
Share
Do you like this story?
KIKUNDI kinachodaiwa kuwa Panya Road kimetikisa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupora mali, kujeruhi watu na kuzua sintofahamu katika maeneo ya jiji hilo wakiwa na mapanga mikononi.
Maeneo yaliyokumbwa na dhooruba hiyo ni pamoja na Sinza, Tandale, Mwananyamala na maeneo mengineyo usiku wa kuamkia leo. Maduka na baa zilifungwa na kupelekea polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa kimakundimakundi.
Imeelezwa kuwa fujo zilianzia mchana jana baada ya kiongozi wa Panya Road aitwaye Diamond kuuawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga.
Baada ya kumzika mwenzao jana Mburahati Jijini Dar, vijana hao wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo.
Usiku ulipoingia wa jana wakaanza kazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Jiji la Dar.
Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia matukio hayo wanadai vijana hao walikuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na walivamia maeneo kadhaa zikiwemo baa.
Wateja waliokuwa katika baa ya Calabash iliyopo maeneo ya Mpakani, Mwenge walilazimika kuacha vinywaji vyao na kukimbia hovyo huku wengine wakikanyagana na kukatwa na vipande vya chupa kwa kile kilichodaiwa kuwa vijana hao walikuwa wanakatiza maeneo hayo japo hawakuingia ndani.
Baada ya tukio hilo wateja wengi waliamua kurudi majumbani kutokana na baadhi yao kujeruhiwa na vipande vya chupa wakati wakikimbia.
0 Responses to “ PANYA ROAD WATIKISA JIJI LA DAR”
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tweets by @FahariNews
More to Read
Buzz
Twitter
Facebook
RSS
Email
Must Read
Popular Posts
MARIE STOPES LAUNCHES MWENGE CALL CENTRE
Marie Stopes Tanzania (MST) re-opened its newly refurbished Mwenge Hospital located at Plot number 421 & 422, Kinyonga Stre...
Kevin De Bruyne amjaza kiburi Pep Guardiola
Meneja wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amemsifia bila kificho kiungo Kevin De Bruyne,...
UNICEF YAUPONGEZA UONGOZI WA MKOA WA MBEYA KWA USHIRIKIANO NA USIMAMIZI WA MIRADI
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amosi Mkalla azindua mradi wa mpango wa Afya na ujasiriamali kwa vijana Picha ya Pamoja ...
Rayvanny - Unaibiwa ( Official Video music )
WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI MBEYA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA Mwonekano wa Gari aina ya Coaster iliyopata ajali. ...
0 Responses to “ PANYA ROAD WATIKISA JIJI LA DAR”
Post a Comment