Friday, February 6, 2015

WANAWAKE WAJANE WA KIMASAI WAANGUA VILIO HUKO MOROGORO




Wanawake wajane ambao ni Wafugaji jamii ya Kimasai, wamejikuta wakiangua kilio katika kituo cha Polisi Mvomero, mkoani Morogoro baada ya kukabidhiwa idadi pungufu ya ng’ombe zilizokamatwa baada ya kuporwa na kundi la ulinzi wa jadi la wakulima.

Walinzi hao wa jadi kutoka katika kijiji cha Dihombo, lilivamia Kijiji cha Kambala ambacho wanaishi wafugaji hao na kupora ng’ombe 145 kwa madai kuwa wafugaji wa kijiji hicho kuwapora wakulima wenzao pikipiki tatu na kusababisha uhalibifu wa trekta wakati wakielekea shambani katika bonde la Mgongola na pikipiki hizo kutelekezwa porini.

Mmoja wa wanawake hao, Belitha William, alisema akiwa kijijini  Kambala akiendelea na shughuli za kuchunga mifugo yake, ghafla alivamiwa na kundi la vijana wenye silaha za jadi maarufu kama muano na kupora ng’ombe wake wapatao 145 pamoja na ndama na kuondoka nao.

Mfugaji huyo alisema alipoifuatilia mifugo hiyo alielezwa inalindwa na kundi la walinzi wa jadi mpaka pale wafugaji wa jamii hiyo ya kimasai watakaporudisha pikipiki walizopora wafugaji wenzao.

Hata hivyo, alisema baadaye mifugo hiyo ilipelekwa ofisi ya Tarafa ya Mvomero kwa ajili ya kupigwa faini mifugo hiyo kuzurura katika mashamba huku mingine ikiwa haipo.
Kwa upande wao, wakulima walioporwa pikipiki hizo, Fabian Clement pamoja naFrancis Boniface, wakielezea tukio la kuporwa pikipiki hizo, walisema kwa nyakati tofauti kuwa wakati wakielekea katika mashamba ya bonde la Mgongola kwajili ya kuwapelekea chakula wenzao, waliona kundi kubwa la wafugaji jamii ya Wamasai wakiwa na silaha za jadi pamoja na bunduki  likiwafuata ndipo walipokimbilia porini.

0 Responses to “WANAWAKE WAJANE WA KIMASAI WAANGUA VILIO HUKO MOROGORO ”

Post a Comment

More to Read