Monday, March 2, 2015
MBUNGE ADUWAZA WAPIGA KURA WAKE KWA KUPIGA MAGOTI MBELE YA WAZIRI MKUU.
Do you like this story?
Katika hali
isiyokuwa ya kawaida Mbunge wa Jimbo la Songwe Mheshimiwa PhilIp Mulogo
ameduwaza wananchi na wapiga kura wake wa jimbo lake la songwe kwa
kitendo chake cha kupiga magoti mbele ya waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa
lengo la kumshinikiza waziri huyo kutoa tamko juu ya lini barabara ya Mbalizi
chunya itakamilika kwa kuwekewa lami.
Hatua hiyo
ilikuja katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mbuyuni
Kata ya Gua jimbo la Songwe ambapo mbunge alitakiwa kutoa neno la shukrani na
kusalimia wananchi mara baada ya waziri mkuu kudhuru katika halmashauri
hiyo ya chunya ikiwa ni sehemu yake ya ziara iliyolenga kutembelea shughuli
mbalimbali za kimaendeleo zinazotekelezwa na serikali pamoja na washirika wa
maendeleo katika mkoa wa mbeya.
Mbunge huyo
mara baada ya kutoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu ghafla alipiga magoti na
kutoa maneno ya huruma kwa kumtaka Waziri Mkuu Pinda kutoa tamko kwa
wananchi juu ya lini barabara ya Mbalizi Mkwajuni itakamilika kwa
wakati na kuondoa kero kwa wananchi wa jimbo lake hali ambayo iliibua mshangao
mkubwa kwa wananchi na wapiga kura wake.
Akiongea mara
baada ya kupiga magoti huku akimtazama Mheshimiwa Pinda alisema kuwa
amekuwa na mtihani mkubwa kwa wananchi wake kuhusiana na kuanza kwa
ujenzi wa barabara hiyo ambayo imekuwa ikizungumzwa mara kwa mara na serikali
kuwa ipo katika mikakakati ya kujengwa.
Amesema kero
kubwa waliyo nayo kwa sasa wananchi wa jimbo hilo ni ubovu wa barabara hiyo
kwani ndio kiungo kikubwa cha kusukuma maendeleo katika jimbo lake la Songwe .
Pamoja na
kuibua hoja hiyo Pia mheshimiwa Mulugo alimuomba Mheshimiwa waziri Mkuu
kulipa nguvu za kutosha suala la uanzishwaji wa Wilaya katika jimbo hilo ambalo
makao makuu yake yamependekezwa kuwa Mkwajuni
Akizungumzia
hoja hizo za Mbunge kwa kuanza na suala la barabara Mheshimiwa Pinda
alisema tayari hatua za awali zimekwisha fanyika kwa kwa kuufanyika
upembuzi yakinifu hivyo amewataka wananchi wa jimbo la songwe pamoja na mbunge
huyo kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea na mchakato huo.
Amesema pamoja
na juhudi hizo pia atajalibu kuzunguzma na Waziri Magufuli ili kufahamu kwa
kina juu ya kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo ya Chunya Mbalizi yenye kilomita
60 .
Kuhusiana na ombila
kuanzishwa kwa Wilaya katika jimbo hilo Waziri Mkuu Pinda amesema tayari
wamekwisha pokea ombi ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) cha Mkoa wa
Mbeya yanayopendekeza mkoa huo ugawanywe na kupata mikoa miwili ya Mbeya na
Songwe.
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda amesema Serikali imeridhia maombi hayo kutokana na ukubwa wa mkoa
huo ambao una kilometa za mraba 63,000 ambapo nusu yake ni Wilaya ya Cunya.
Amesema kamati
hiyo imeshauri mkoa huo ugawanywe katika wilaya nne nne ambapo mkoa mpya wa
Songwe utakuwa na wilaya za Ileje, Momba, Mbozi na Chunya.
Alisema katika
kikao hicho ilikubaliwa kwamba makao makuu ya wilaya mpya ya Songwe yatakuwa
Mkwajuni .
. “Nimekubali
maombi haya kwa sababu yatapunguza gharama za uendeshaji, na kama itashindikana
kupata wilaya mpya basi itabidi tuwape Halmashauri ya Songwe,” alisema.
Mkoa wa Mbeya
una wilaya nane ambazo zimegawanyika katika tarafa 27, kata 262, vijiji 842 na
mitaa 252. Idadi ya wakazi kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012
ni 2,707,410.
Mwisho
JAMIIMOJABLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBUNGE ADUWAZA WAPIGA KURA WAKE KWA KUPIGA MAGOTI MBELE YA WAZIRI MKUU.”
Post a Comment