Thursday, March 5, 2015
UFAFANUZI JUU YA HALI YA AFYA YA NAIBU SPIKA WA BUNGE MHE. JOB NDUGAI.
Do you like this story?
Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa
kwenye Mitandao ya kijamii kuhusu hali ya Afya ya Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job
Ndugai.
Ofisi ya Bunge inapenda kuutangazia umma na Wananchi wote kuwa, taarifa hizo zinazosambazwa katika baadhi ya Mitandao si za kweli, bali ni uzushi mtupu.
Ukweli ni kwamba Naibu Spika wa Bunge,
Mhe. Job Ndugai ni Mzima wa afya na hivi sasa yuko jimboni kwake Kongwa, Mkoani
Dodoma akifanya maandalizi ya Mwisho ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg.
Abdulrahman Kinana itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii na hasa Jimboni Kongwa,
Dodoma.
Ofisi ya Bunge inapenda kuwatoa hofu
Wananchi wote na kuwataka kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa si za kweli bali ni
uvumi unaonezwa na watu wachache wenye nia ovu ya kujenga hofu miongozni mwa
Wananchi kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha tunapenda kutoa rai kwa watu wote
kuacha kusambaza taarifa hizo potofu na badala yake kama kuna taarifa zozote
kuhusu Ofisi ya Bunge au Viongozi wake wafanye jitihada za kuthibitisha taarifa
hizo kwenye Mamlaka husika kabla za kuzisambaza.
Ofisi ya Bunge inao utaratibu rasmi wa
kutoa taarifa muhimu kwa wananchi na umma kwa ujumla, hivyo si vyema kwa watu
kusambaza taarifa potofu kuhusu Bunge na viongozi wake ambazo zinaweza kuleta
usumbufu miongoni mwa Viongozi na baadhi ya wananchi.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
4 MACHI 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UFAFANUZI JUU YA HALI YA AFYA YA NAIBU SPIKA WA BUNGE MHE. JOB NDUGAI.”
Post a Comment