Thursday, May 21, 2015
MBUNGE ATAKA MKUU WAKE WA WILAYA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI WAJIUZULU HARAKA
Do you like this story?
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini amewajia
juu Mkuu wa Wilaya ya Rombo,Lembrise
Kipuyo na Mwenyekiti wa Halmashauri
ya wilaya ya hiyo, Anthony
Tesha akiwataka wajiuzulu nyadhifa zao kwa
kushindwa kusimamia sheria wilayani humo.
Selasini alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumzia
taarifa ya wanawake wa Rombo inayodai kwamba wanakodi wanaume kutoka Kenya ili
wafanye nao tendo la ndoa.
Juzi, gazeti hili liliripoti habari iliyomkariri Mkuu wa
Wilaya kuwa baadhi ya wanawake wilayani humo, hukodi wanaume kutoka Kenya kwa
ajili ya kufanya nao tendo la ndoa baada ya waume zao kupoteza nguvu kutokana
na ulevi.
Eneo ambalo limeathirika zaidi na unywaji wa pombe haramu na
zinazotengenezwa kiholela bila viwango ni la Kikelelwa lililopo mpakani mwa
Kenya na Tanzania.
Taarifa hiyo ilimnukuu Kipuyo wakati wa ufunguzi wa kikao
cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo na kuitaja Kikelelwa kama eneo
linalohitaji kutazamwa kwa jicho la pekee.
“Imefikia mahali wanaume wengi
wanashindwa kumudu kufanya tendo la ndoa na kuwalazimu wanawake wao kukodi
wanaume kutoka nchi jirani ya Kenya kwa ajili ya tendo hilo,” Kipuyo.
Kauli hiyo iliungwa mkono na baadhi ya wanawake
waliozungumza mbele ya mkuu huyo wa wilaya katika operesheni ya kukamata pombe
haramu ya gongo kijijini hapo iliyofanyika wiki mbili zilizopita.
Jana, Selasini alikanusha vikali taarifa hizo akidai kuwa
siyo sahihi kuwajumuisha wanaume wote wa jimbo lake na ulevi huo au wanawake
wote.
“Hiyo kauli haina utafiti wala
haijaonyesha ni wanaume wangapi Rombo wana tatizo hilo au ni wanawake wangapi
waume zao wana shida hiyo. Siyo sahihi kutoa kauli ya jumla,” .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBUNGE ATAKA MKUU WAKE WA WILAYA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI WAJIUZULU HARAKA ”
Post a Comment