Friday, May 22, 2015
WANAWAKE KUTOTUMIA WHATSAPP, CHECHNYA.
Do you like this story?
Kiongozi wa Chechnya
Ramzan Kadyrov amewataka wanaume kuwazuia wake zao kutumia mtandao wa kijamii
wa WhatsApp baada ya mada ya ndoa ya lazima kusambaa katika ujumbe mfupi wa
simu.
Kadyrov amekaririwa akisema "wafungie
ndani, msiwaache wakatoka nje, kwa hiyo hawatatuma chochote,"
Bwana Kadyrov mapema aliunga mkono ndoa ya
afisa wa Polisi kumwoa msichana wa miaka 17, japokuwa alikuwa tayari ameolewa,
katika tukio la ukiukaji wa sheria za Urusi.
Mnadhimu wake wa kijeshi tangu wakati huo
alipendekeza kuhalalisha ndoa ya zaidi ya mke mmoja nchini Chechnya.
Bwana Kadyrov, kiongozi wa kimla na mshirika
wa karibu wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, katika miaka ya karibuni alipiga
marufuku kuwachukua kwa nguvu wanawake kwa ajili ya kufunga nao ndoa za umri
mdogo.
Pia anafikiriwa kuwa anapendelea ndoa za wake
wengi. Msaidizi wake mkuu Magomed Daudov anasema: "hiyo yote inaendana na
Sharia. Lakini kama mwanaume anaweza kuhudumia zaidi ya mke mmoja, kwa nini
asioe wengi?" Watu wengi katika jamhuri ya ya Urusi ya Chechnya, ni
Waislamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAWAKE KUTOTUMIA WHATSAPP, CHECHNYA.”
Post a Comment