Wednesday, May 20, 2015
MICHUANO YA COSAFA YAANZA AFRICA KUSINI.
Do you like this story?
Michuano ya kumi na tano ya Baraza la Vyama
vya Mpira wa Miguu kusini mwa Afrika,COSAFA imezikutanisha timu za ukanda huo
nchini Afrika Kusini. Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Jumapili mei 17 na
itakamilika mei 30
Timu 12 kati ya 14 kutoka nchi wanachama wa
COSAFA tayari zipo nchini Afrika Kusini kuchuana katika mashindano hayo. Angola
na Comoro ambazo ni wanachama wa COSAFA hazikuweza kushiriki mwaka huu.
Nafasi zao zimechukuliwa na Ghana iliyofikia
fainali za michuano ya Caf ya mwaka huu na Tanzania kutoka ukanda wa Afrika
mashariki na kati ikiwa mwanachama wa CECAFA.
Timu nane zenye viwango vya chini kwa ubora
kwa mujibu wa takwimu za FIFA kwa mwezi Februari, zimepangwa katika makundi
mawili yenye timu nne kila moja, Tanzania ikiwemo katika michuano hiyo.
Kundi A lina timu za Zimbabwe, Namibia, Seychelles
na Mauritius. Ambapo kundi B lina timu za Madagascar, Lesotho, Swaziland na
Tanzania.
Katika kundi A Zimbabwe inaoongoza kundi hilo
kwa kujikusanyia pointi sita baada ya michezo miwili ikifuatiwa na Namibia
yenye pointi nne. Seychelles ni ya tatu na pointi moja. Mkiani ni Mauritius
ambayo haina pointi.
Na katika kundi B, Madagascar na Swaziland
zote zina pointi tatu, huku Lesotho na Tanzania zikiwa mikono mitupu.
Tanzania leo,Jumatano inarusha karata yake ya
pili kwa kupambana na Madagascar baada ya kucharazwa bao 1-0 na Swaziland
katika mchezo wake wa kwanza.
Timu za juu katika kila kundi zitasonga mbele
hatua ya mtoano, ambapo timu sita za viwango vya juu zitaingia katika
mashindano hayo yakiwa katika hatua ya robo fainali na kuendelea. Afrika Kusini
kutokana na ubora wake itapambana na Botswana hatua ya robo fainali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MICHUANO YA COSAFA YAANZA AFRICA KUSINI.”
Post a Comment