Sunday, May 17, 2015
STARS IKIIKABILI SWAZILAND KESHO COSAFA, JULIO APASUKA YA MOYONI....
Do you like this story?
TIMU ya soka ya
taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kesho itacheza mchezo wake wa kwanza wa
kombe la Cosafa dhidi ya Swaziland katika uwanja wa Royal Bafokeng pembeni
kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika
Kusini na saa 2:30 kwa saa za Afrika mashariki.
Kuelekea katika
mechi hiyo kocha msaidizi wa zamani wa Taifa Stars na sasa kocha mkuu wa
Coastal Union, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ amefurahishwa na uteuzi wa baadhi ya
wachezaji vijana, lakini amesema wangekuwa wengi zaidi kuliko wakongwe ili
kujenga timu ya baadaye.
“Kilichonifurahisha
ni uteuzi wa baadhi ya wachezaji wadogo kama Ajib (Ibrahim), Ndemla (Said),
wachezaji kama hawa wangekuwa wengi katika kipindi hiki cha mashindano,
hakika ingetusaidia kutuweka vizuri katika mashindano yajayo”. Amesema Julio na
kusisitiza:
“Ukiangalia
timu za wenzetu utakuta kuna vijana wengi kwenye timu kuliko wakongwe, kwa
mfano nchi kama Ivory Coast, ilikuja hapa (Tanzania) na timu ya vijana kama
vile Kipre Tchetche na Michael Balou wa Azam fc, leo hii wanatusumbua katika
ligi ya nyumbani, kwahiyo tungechukua wachezaji wengi wadogo kuliko wakongwe
kama Aggrey Morris, vijana wakipata uzoefu katika mashindano kama hayo wanaweza
kutengeneza mpira wao. Wachezaji wakongwe wangetolewa".
Kuhusu mechi ya kesho, Julio amesema: "Mechi ya kesho mwalimu amesema maandalizi ni mazuri, kama ni mazuri kweli basi tusubiri, naamini wachezaji watafanya kazi yao, kwasababu walifanya mazoezi vizuri, walipata uwanja mzuri"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “STARS IKIIKABILI SWAZILAND KESHO COSAFA, JULIO APASUKA YA MOYONI....”
Post a Comment