Tuesday, May 19, 2015
WAENDESHA BODABODA DAR WACHOSHWA NA MANYANYASO....WAAMUA KUFANYA MAANDAMANO
Do you like this story?
Kundi la waendesha pikipiki maarufu kama boda boda kutoka
vituo vya kawe,bondeni hadi Tangibovu wamelalamikia na kupinga kukithiri kwa
uonevu wa makundi yanayojiita ulinzi shirikishi,polisi jamii na Tambaza dhidi
yao wakidai kuwatoza fedha nyingi mara kwa mara kama adhabu za usalama
barabarani ya kati ya shilingi elfu hamsini hadi laki moja bila ya stakabadhi.
Katika malalamiko hayo walieleza wazi kutokuwa na ugomvi na
askari polisi wa usalama barabarani zaidi ya makundi hayo ambayo hayana sare
wala vitambulisho ambao kuwakuta katika makutano ya barabara na kuwanyang”anya
funguo kwa maelezo ya kutoa fedha hizo kabla ya kupelekwa kwenye vituo vya
polisi na wakati mwingine huwafanya kusababisha ajali kwa hofu ya kuwakimbia.
Katika tamko lao lilitolewa na mwenyekiti wao Bw.
Kalos Mbwalo wanamuomba mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini pamoja na
serikali kutambua sekta hiyo kuwa ni ajira kama ajira zingine na kutazama upya
ushiriki wa makundi hayo katika shughuli za usalama barabarani kutokana na
kuonekana kujitwisha majukumu ya polisi huku wakiwa hawana weledi wa kutosha na
kujikuta wakigeuza shughuli hizo kuwa miradi ya kujinufaisha na hofu ya vikundi
hivyo kuwa nyuma ya baadhi ya viongozi.
mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kiondondoni
kamanda Awadhi Haji Akiongea kwa njia ya simu ambaye pamoja na kueleza mbinu za
kikosi chake kufanyakzi kwa kutumia askari waliovaa kiraia amesema kwa
malalamiko hayo ipo haja ya madereva hao kufika ofisi kwao kutoa ushirikiano
ili waweze kubaini watu hao wanaolipaka matope jeshi la polisi na kuwachukulia
hatua za kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAENDESHA BODABODA DAR WACHOSHWA NA MANYANYASO....WAAMUA KUFANYA MAANDAMANO ”
Post a Comment