Thursday, June 4, 2015
AFISA WA FIFA AKIRI ALIPOKEA RUSHWA.
Do you like this story?
Wizara ya Sheria ya
Marekani imechapisha taarifa inayoelezea jinsi Afisa wa zamani wa FIFA Chuck
Blazer alivyokiri kuwa yeye pamoja na wenzake walipokea rushwa ikiwa ni pamoja
kuichagua Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa fainali ya kombe la dunia mwaka 2010.
Katika taarifa hiyo imeweka wazi mtandao wa
malipo ya rushwa ulivyokuwa ukifanywa ndani ya shirikisho la soka duniani FIFA,
taarifa zinazoegemea uchunguzi uliofanywa na shirika la kijasusi la Marekani
FBI.
Taarifa hiyo ambayo inamwelezea Afisa humo wa
zamani wa Fifa Chuck Blazer kukiri kupokea rushwa sasa huenda ikaibua mengi
kwenye kashfa ya rushwa inayoindamana shirikisho la FIFA.
Mmerakani huyo kwenye taarifa hiyo inadai
alikuwa ni mmoja wa watu waliosuka mipango ya kupokea rushwa katika tukio
jingine la fainali la kombe la dunia 1998.
Taarifa za Kukiri zipo katika maandishi
wakati wa kesi yake mwaka 2013 wakati kesi yake ilipokuwa akisikilizwa katika
mahakama ya Easten New York huko Marekani ambapo alikiri makosa kumi yaliyokuwa
yanamkabili.
Blazer alikuwa afisa wa ngazi juu wa FIFA
eneo la kanda ya Amerika Kaskazini na Kati na ukanda wa nchi Caribbean kuanzia
mwaka 1990 hadi mwaka 2011.
Marekani imefungua kesi ya rushwa
inayowakabili maafisa wa FIFA jambo lililofanya Rais wa FIFA Sepp Blatter
kuamua kutangaza kujiuzulu.
Mwendesha mashtaka wa Marekani wiki iliyopita
aliwashtaki maafisa 14 wa ngazi wa juu wa FIFA tuhuma za rushwa, kutakatisha
fesha,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AFISA WA FIFA AKIRI ALIPOKEA RUSHWA.”
Post a Comment