Monday, November 2, 2015
.CCM MBEYA YAKIRI NA KUKUBALI KUPOTEZA MAJIMBO 4 NA HALMASHAURI MBILI
Do you like this story?
Chama
cha mapinduzi mkoani Mbeya kimekiri na kukubali kupoteza majimbo manne ya uchaguzi
na halmashauri mbili ambazo zimenyakuliwa na vyama vya upinzani kwenye uchaguzi
mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, huku kikimpongeza rais mteule wa awamu
ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kutangazwa mshindi wa ngazi ya urais kwenye
uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa
chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi ndiye ambaye ametoa tamko hilo
kwa niaba ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya
makada wa CCM wamesema kuwa ushindi wa Dk. Magufuri ni ushindi wa watanzania wote
kwa kuwa ni mtu mwadilifu na mwenye uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo
kutokana na tabia yake ya kupenda kuchapa kazi.
Baadhi ya
wananchi wamesema kuwa wanamtarajia rais Magufuri kuteua wasaidizi wake walio
makini ili aweze kukidhi matarajio ya wanananchi huku pia wakitoa tahadhari kwa
viongozi wazembe serikalini kuwa wajiandae kwa mabadiliko na kuanza kujituma
kufanya kazi baada ya kuapishwa kwa Dk. Magufuri kuwa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “.CCM MBEYA YAKIRI NA KUKUBALI KUPOTEZA MAJIMBO 4 NA HALMASHAURI MBILI”
Post a Comment