Tuesday, January 19, 2016
AIRTEL MKWANJIKA YAPATA WASHINDI, NANE WAJIZOLEA FEDHA, MBEYA
Do you like this story?
Iddi Yusufu akiendelea kuokota fedha katika boksi kwenye shindano la kwangua ushinde na Airtel Mkwanjika(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akipewa maelezo kabla ya kuingia kwenye boksi la kuokota fedha katika shindano la kwangua ushinde(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mshindi Jotham Mwainyekule akijaribu bahati yake kama anaweza kuokota fedha zote ambazo ni shilingi Milioni Moja anazopaswa kuziokota kwa muda wa sekunde 60.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya wakishuhudia shindano la Kwangua ushinde la Airtel Mkwanjika(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
PROMOSHENI inayoendeshwa na Kampuni ya Simu za mkononi ya
Airtel inayojulikana kwa jina la Kwangua ushinde na Airtel Mkwanjika imetua
katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini ambapo washindi nane wamepatikana na
kujizolea fedha taslimu.
Zoezi la kuwapatia zawadi washindi hao lilifanyika jana
katika ofisi za Kanda za Airtel zilizopo Uhindini Jijini Mbeya na kushuhudiwa
na wakazi wa Jiji hilo kutokana na zoezi hilo kufanyika katika maeneo ya wazi.
Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Nyanda za juu kusini,
Straton Mushi alisema tangu shindano hilo lianze mwezi Disemba mwaka jana nchi
nzima wateja wengi wamejitokeza na kujizolea fedha lukuki ambazo zimekuwa
zikiwasaidia katika kuboresha hali yao ya kiuchumi kwa kuongeza vipato vyao.
Alisema hakuna masharti yoyote ya mteja kujishindia bali
anachopaswa ni kununua vocha na kuikwangua kasha kuijaza kwenye simu yake ya
Airtel anakuwa ameingia moja kwa moja kwenye shindano ambapo baada ya
kuchaguliwa huingizwa kwenye boksi maalum lenye fedha taslimu shilingi Milioni
moja ambazo hupulizwa na upepo hivyo kasi ya mteja kuokota fedha ndizo zinakuwa
zawadi yake.
Aliwataja washindi walioshiriki kujiokoteza fedha kwa Kanda
kuwa ni pamoja na Ismail Mwaswale (Sumbawanga) ambaye kwenye boksi alijiokotea
jumla ya shilingi 920,000 kwa muda wa sekunde sitini akifuatiwa na Iddi Yusufu
(Iringa) aliyeokota shilingi 750,000 na Jotham Mwainyekule mkazi wa Mbozi
aliyepata shilingi 730,000/=.
Aliwataja washindi wengine kuwa ni Kazembe Salamanda Mkazi
wa Ruvuma, Onesmo Lubaga mkazi wa Iringa, Tonny Moris Mkazi wa Mbeya, Bahati
Muhawala mkazi wa Mbeya na Thomas Baraka mkazi wa Rukwa ambao viwango vyao
havikujulikana mara moja.
Wakizungumza baada ya kumalisha shindano hilo washindi hao
walitoa wito kwa watanzania kuiamini Airtel na kuitumia kwa kuwa huduma zao ni
za kweli na uhakika tofauti na madai ya wengi kuwa promosheni hizo ni danganya
toto.
Ismaila Mwaswale(43)Mkazi wa Sumbawanga na mfanyabiashara
mdogo alisema baada ya kupigiwa simu kwamba ameshinda hakuamini hadi pale
alipotumiwa nauli ya kuja kushiriki zoezi hilo mkoani Mbeya.
Alisema fedha alizopata zitamsaidia kuongeza mtaji wa
biashara yake ambayo imekuwa ikisuasua kutokana na mtaji mdogo huku fedha
zingine akizielekeza kulipia karo za watoto wanaosoma shule binafsi.
Iddi Yusuph (26) mkazi wa Iringa alisema ni vema Watanzania
na wateja wa Airtel wakaamini kuwa kichezo hiyo ipo na inafanyika kweli wala
sio utapeli na haifanyiki kwa kujuana na watumishi wa airtel kwani yeye
mwenyewe ameshinda pasipo kutoa chochote wala kujuana na mtumishi yeyote.
Baadhi ya mashuhuda wa mashindano hayo walisema ni jambo
zuri linalofanywa na Kampuni ya Airtel kwa kuweka mashindano ya wazi ambapo
kila mtu anaona namna mshiriki anavyohangaika kuokjota fedha kutoka kwenye
boksi na kwamba hali hilyo huonesha kuwa hakuna upendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AIRTEL MKWANJIKA YAPATA WASHINDI, NANE WAJIZOLEA FEDHA, MBEYA”
Post a Comment