Wednesday, January 20, 2016

SERIKALI YATOA AMRI WAKUU WA SHULE KIGOMA WARUDISHE MICHANGO YA WANAFUNZI


Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Gerrard Guninita aliyesimama. (Picha na Emmanuel Senny).


Na Emmanuel Senny, Kigoma
Baadhi  ya  wakuu wa shule za sekondari na msigi katika Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wamepewa wiki moja wawe wamerusidisha pesa walizowachangisha wazazi ikiwa ni kitendo cha kukiuka agizo la Rais kuhusu utoaji elimu bure.

Akizungumza katika kikao cha madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Vijijini mkoani hapa. Mkuu wa Wilaya hiyo Gerrard Guninita alisema kuwa, walimu hao walikiuka agizo la Rais kwa kuwatoza wanafunzi pesa za ada na michango mingine.

Kwa kuthibitisha suala hilo Guninita alisema kuwa, baada ya shule kufunguliwa alipita katika baadhi ya shule na kugundua kuna baadhi ya walimu wanachukua pesa za kuwaandikisha wanafunzi sambamba na  michango mingine ikiwemo komputa.

“Sasa kwakuwa walimu hao wanafanya hivyo huku wakiwa wanajua ni makosa, ninawapa wiki moja wawe wamerudisha pesa hizo kwa wazazi wote na endapo wasipofanya hivyo ndani ya wiki moja hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema Guninita.

Aidha Guninita aliwataka  madiwani katika wilaya hiyo kuhakikisha wanawaelimisha wazazi kuwapeleka watoto wao shule kutokana na vikwazo vilivyotolewa ikiwemo ada na michango mingine.

“Kwa mzazi atakae shindwa kumpeleka mtoto shule kwa sababu zake binafsi hatuta mvumilia tutamchukulia hatua hivyo  ninaomba wazazi wote muhamasike kuwapeleka shule watoto wenu,” aliongeza  Guninita.

0 Responses to “SERIKALI YATOA AMRI WAKUU WA SHULE KIGOMA WARUDISHE MICHANGO YA WANAFUNZI”

Post a Comment

More to Read