Tuesday, January 26, 2016
DARAJA LA KIGAMBONI KUANZA KUTUMIKA MACHI MOSI
Do you like this story?
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sehemu ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga amesema daraja la Kigamboni litaanza kutumika kuanzia Machi mwaka huu.
Akizungumza
mara baada ya kukagua hatua za ujenzi wa daraja hilo Eng. Nyamhanga amemtaka
msimamizi wa ujenzi huo kuhakikisha hatua ya ujenzi iliyobaki inakamilika
katikati ya mwezi februari na kuanza kazi mwanzoni mwa mwezi Machi.
“Hakikisheni
Machi mosi magari yaanze kupita rasmi kwenye daraja hili na hivyo kufungua
ukurasa mpya kwa wakazi wa Kigamboni ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa
na msongamano katika eneo la Magogoni”,
amesema Eng. Nyamhanga.
Eng. Nyamhanga
amesisitiza kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuunganisha daraja la
Kigamboni na barabara ya Charambe,Mlandizi hadi Chalinze ili kupunguza
msongamano wa magari katikati ya Jiji.
Amemtaka meneja
wa mradi wa ujenzi wa daraja hilo toka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng.
John Msemo kuhakikisha anatafuta Wakala makini atakayesimamia na kuendesha
mradi huo.
Daraja la
Kigamboni lenye urefu wa mita 680, unasimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano linatarajiwa kuishi zaidi ya miaka 100 na kuwa na uwezo wa
kupitisha mizigo ya tani 56 zinazokubalika katika nchi za jumuiya ya madola.
IMETOLEWA
NA ;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ DARAJA LA KIGAMBONI KUANZA KUTUMIKA MACHI MOSI”
Post a Comment