Tuesday, January 26, 2016
HAYA NDIO MAMBO 8 YATAKAYOWASHA MOTO BUNGE LA 11 LINALOANZA LEO
Do you like this story?
Kikao cha pili
cha Bunge la kumi na moja linalotarajiwa kuwa na ushindani mkali wa hoja kati
ya wabunge wa vya upinzani vinavyounda Ukawa na wabunge wa CCM kimeanza leo
mjini Dodoma huku mambo 8 muhimu yakitarajiwa kuibua mjadala mkubwa.
Jambo
la kwanza ni kujadili hotuba ya Rais John
Magufuli aliyoitoa bungeni hapo mwaka jana katika kikao cha kwanza cha bunge
hilo. Hapo suala la kupambana na ufisadi linatarajia kuleta hoja nzito zaidi
kutoka kila upande. Hotuba ya Rais ilisifiwa na takribani kila mwananchi pamoja
na wanasiasa mbalimbali.
Pili, Kurudiwa kwa uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Hili ni suala nyeti
na linalopaswa kubebwa kwa uangalifu mkubwa.
Wabunge wa
Ukawa na CCM wanatarajiwa kurusha makombora yao ya hoja na maoni katika
kusaidia namna ya kupata muafaka. Bila shaka hapo mengi yataibuka na huenda
kukawa na mgongano mkubwa wa hoja na mawazo.
Tatu, Zoezi la Bomoabomoa pia linaweza kupewa nafasi yake katika
Bunge hilo hususan katika utekelezaji wake na mapungufu yaliyojitokeza.
Nne,Maazimio ya Bunge juu ya sakata la ESCROW linaweza kuwa mada
moto zaidi katika bunge hilo kwani tayari kumekuwa na vutankuvute kabla ya
Bunge.
Mbunge wa jimbo
la Ubungo Saed Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ambao ni mahasimu
wa kisiasa wameonekana kuwa na nia moja katika kulirudisha bungeni sakata la
ESCROW. Mmiliki wa Kampuni ya IPTL/PAP, Harbinder Singh Sethi amepinga
mahakamani kurudishwa bungeni kwa sakata hilo lakini Zitto amesisitiza kuwa mtu
binafsi hawezi kulizuia Bunge kutekeleza majukumu yake.
Tano,Utekelezaji wa sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi
hadi kidato cha nne pia ni suala ambalo litaleta mjadala katika Bunge hilo, kwa
kuzingatia changamoto zilizoanza kuripotiwa.
Sita,Uteuzi wa wajumbe wa kamati za Bunge ambao vyama vya
upinzani vinavyounda Ukawa vimeulalamikia na hata kutishia kuususia unatarajiwa
kuwa sehemu ya hoja zitakazoleta mjadala mkubwa katika Bunge hilo.
Saba,Ni migogoro iliyoibuka katika chaguzi za Mameya wa majini na
Manispaa pamoja na wenyeviti wa Halmashauri. Waziri wa TAMISEMI atakuwa na kazi
ya kujibu hoja na maswali yatakayokuwa yanaelekezwa kwake kuhusu zoezi hilo.
Nane,
Hoja binafsi za wabunge zinatarajiwa
kuibuliwa na kuleta mjadala mzito kwani tayari baadhi ya wabunge wamekwisha
eleza nia yao ya kupeleka bungeni hoja binafsi kuhusu masuala mbalimbali.
Bunge hili
linatarajiwa kuwa la kipekee na lenye changamoto kubwa kwa kuwa na idadi
kubwa ya vijana na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ambao wameunda umoja wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ HAYA NDIO MAMBO 8 YATAKAYOWASHA MOTO BUNGE LA 11 LINALOANZA LEO ”
Post a Comment