Tuesday, January 26, 2016
LUKUVI: MANISPAA YA ILALA YAPEWA SIKU 30 KUBOMOA GHOROFA LILILOJENGWA CHINI YA KIWANGO
Do you like this story?
Jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi jijini Dar,kama lionekanavyo pichani. |
Sehemu ya jengo ambayo inaonekana imepasuka.(Picha na Emmanue Massaka) |
WAZIRI wa
Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza watendaji wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo
refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indira Ghandhi ndani
ya mwezi mmoja kuanzia sasa.
Lukuvi ametoa
kauli hiyo jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea kwenye ziara fupi katika
Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo nako pia amebaini matatizo mbalimbali
katika sekta ya Ardhi.
“Miezi
sita iliyopita Rais Mstaafu alikuja hapa akaagiza jengo hili libomolewe na nyie
mkajiridhisha kweli lafaa kubomolewa sasa inakuwaje mpaka leo linaendelea
kuwepo? Naagiza mfanye haraka jengo hili ndani ya mwezi mmoja taratibu za
ubomoaji ziwe zimeanza ili kulinusuru taifa kuingia katika janga jingine.”alisema Waziri Lukuvi.
Akiwa bagamoyo
waziri Lukuvi alibaini katika Wilaya ya Bagamoyo upotevu wa viwanja vya wanachi
ambavyo walitakiwa kupewa katika eneo la ukuni ambapo vimetoweka
Mara baada ya
kupata taaarifa hiyo mmoja wa wakaazi wa bagamoyo ambaye alitoa malalamiko juu
ya viwanja hivyo mbele ya mkutano wa hadhara na kutaja kuwa Halmashauri
ilichukua kiasi cha pesa kuanzia laki sita kwa kila mtu mwaka 2005 na kuahaidi
kuwapatia viwanja lakini mpaka leo hawajapewa.
Mara baada ya
kupata taarifa hiyo waziri Lukuvi aliwagiza watendaji wa wilaya hiyo ndani ya
miezi sita wawe wamewapatia wakazi hao viwanja hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ LUKUVI: MANISPAA YA ILALA YAPEWA SIKU 30 KUBOMOA GHOROFA LILILOJENGWA CHINI YA KIWANGO”
Post a Comment