Wednesday, January 20, 2016
DKT. KIGWANGALLA AUNDA KIKOSI KAZI KUBORESHA HUDUMA ZA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)
Do you like this story?
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla. |
Naibu Waziri wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla
ameanzisha kikosi kazi cha watu 24 ambacho kitakuwa na kazi ya kutengeneza
mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Katika taarifa ambayo
imetolewa na Dkt. Kigwangala imeeleza kuwa kazi ya kuanzisha kikosi kazi hicho
ni agizo kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ambaye alimtaka aanzishe kikosi hicho ili
washirikiane kuanzisha mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya
Jamii.
“Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu alinipa
kazi ya kuunda kikosi kazi maalum na kushirikiana nacho kutengeneza mpango
mkakati wa kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),” alisema Dkt. Kigwangalla.
Dkt. Kigwangalla
amewataja wajumbe wa kikosi kazi hicho kuwa ni Prof. Angwara Kiwara, Prof.
Phares Mujinja, Dkt. Francis Frederick, Dkt. Heri Marwa, Dkt. Deogratius Pisa,
Dkt. Amos Kahwa, Irenei Kiria, Semkae Kilonzo, Gemini Mtei, Dkt. Jehovaness
Aikaeli na Obey Assey.
Wengine ni Mathias
Kabunduguru, Dkt. Dereck Chitama, Prof. Flora Kessy, Florence Mwanri, Athuman
Rehani, Maximillian Mapunda, Bedason Shallanda, Daniel Ngowi, Beng' Issa, Edwin
Mikongoti, Hussein Sengu, Dkt. Beatus Leon na Dkt. Pastory Sekule.
Aidha Dkt. Kigwangalla
amewashukuru wajumbe hao kwa kukubali kufanya kazi na wizara ya afya kupitia
mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii bila malipo
yoyote.
Hata hivyo mara baada ya
kuwachagua wajumbe wa kikosi kazi hicho tayari kimependekeza mapendekezo yao
jinsi ya kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii ambayo ni kuipa nguvu kadi ya CHF ili
itumike kwenye mfumo wa Afya mpaka ngazi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa na
vituo vya Jirani na kupandisha kiwango cha kuchangia CHF mpaka 30,000.
Mapendekezo mengine ni
kuweka bei za kukatisha tamaa watumiaji wa huduma za Afya bila kadi ya Bima ya
Afya ama ya CHF na kuwahamasisha waamue kujiunga kuliko kulipa gharama za kila
huduma watakayotumia, kuhamisha Mfuko wa fedha za CHF kutoka Halmashauri na
kuupeleka NHIF ngazi ya mkoa lengo likiwa kumtenganisha mtoa huduma na mteja na
kuweka 10,000 kuwa kiwango cha chini kwa bei za huduma za afya sehemu yoyote
nchini kwa mtu asiye na kadi.
Aidha mapendekezo yao
yatatumika kama serikali itayaridhia na wao wametoa mapendekezo hayo kutokana
na kutambua kuwa Watanzania wapo tayari kulipia huduma za afya kwa bima
ilimradi wawe wanapatiwa huduma bora ambazo zitawaridhisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DKT. KIGWANGALLA AUNDA KIKOSI KAZI KUBORESHA HUDUMA ZA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)”
Post a Comment