Wednesday, January 20, 2016
MGODI PEKEE WA DHAHABU TANZANIA ULIOCHINI YA WAZAWA
Do you like this story?
Mgodi wa Stamigold Biharamulo ni mgodi pekee
hapa nchini unaozalisha dhahabu kwa kusimamiwa na kuendeshwa na Wataalam wa
Kitanzania pekee. Mgodi wa Biharamulo chini ya Meneja wake Mkuu Mhandisi Dennis
Sebugwao,
umeweza kuisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira wakati huo huo
kuiongezea serikali mapato kutokana na kodi mbalimbali zinazolipwa na
Wafanyakazi walioajiriwa (PAYE)
Mbali na kuajiri Wataalam wa fani mbalimbali
mgodi pia unatumia Wakandarasi wa Kitanzania pamoja na kutoa ajira za muda mfupi kwa wakazi wa vijiji vilivyo
jirani na mgodi.
(Mavota & Mkunkwa)
Wengi wa Watanzania wana ile dhana ya kuwa
Watanzania hatuna uwezo wa kusimamia na kuendesha migodi bila kuajiri wataalamu
kutoka nje ya nchi. Mgodi wa Stamigold Biharamulo umedhamiria kuendelea
kudhihirishia Watanzania wenzetu na dunia nzima kwa ujumla kuwa kupitia
wataalamu tulionao nchini kwetu tunao uwezo wa kuzalisha dhahabu bila kutegemea
wataalamu kutoka nje ya nchi.
“Tutaendelea kufanya kazi kwa uadilifu,
weledi, ushirikiano, bila kukata tamaa na bila kushindwa. Daima tutasonga mbele
kurudi nyuma ni mwiko.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MGODI PEKEE WA DHAHABU TANZANIA ULIOCHINI YA WAZAWA”
Post a Comment