Wednesday, January 20, 2016

JK AHANI MSIBA WA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TAA, MHANDISI SULEIMANI SAID SULEIMAN


JK akimpa pole mtoto wa mwisho wa marehemu, Hosam Suleiman Said Suleiman

JK akisalimiana na mdogo wa marehemu, Mhandisi Nasiri Said Suleiman.

JK akisalimiana na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Bw. Ramadhan Maleta.

JK akimpa pole mama wa marehemu.


RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na watoto watatu wa marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman, aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Nchini, TAA, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, jana Januari 19, 2016 kutoa mkono wa pole. Marehemu Suleiman alifariki Jumatatu Januari 18, 2016 wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya hindi na tayari amezikwa. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said).

Akisaini kitabu cha maombolezo.

Mama Salma Kikwete, akitoka nyumbani kwa marehemu Mhandisi Suleiman Said, baada ya kuhani msiba wake Januari 19, 2016


RAIS mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, jana Januari 19, 2016 amehani msiba wa aliyekuwa Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman.

Dkt. Kikwete aliwasili nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, akifuatana na mkewe Mama Salma Kikwete majira ya saa 10:30, akitokea kijijini kake Msoga mkoani Pwani.

Baada ya kiwasili, nyumbani kwa marehemu Rais mstaafu alipokewa na mdogo wa marehemu, Mhandisi, Nasiri Said Suleiman, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw.  Laurent Mwigune, Mkurugenzi wa Sheria na Mawasiliano ya umma, Bw. Ramadhan Maleta, maafisa wa TAA, na wanafamilia wengine na kwenda moja kwa moja kuweka saini kitabu cha maombolezo.

Baada ya kufanya mazungumzo kwa muda, Watoto wawili wa marehemu ambao wanasoma nje ya nchi nao waliwasili na kupata fursa ya kusalimiana na Rais mstaafu, Dkt. Kikwete.

Watoto hao ni pamoja na mtoto mkubwa wa marehemu, Mohammed Said Suleiman, na mdogo wake Said Suleiman Said.

Baadaye Rais Kikwete alikwenda kusaliamiana na mama mzazi wa marehemu, mke wa marehemu na wafiwa wengine na kisha yeye na msafara wake kuondoka majira ya saa 11 jioni.

Mhandisi Suleiman Said Suleima, alifariki dunia Januari 18, 2016 majira ya asubuhi wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya hindi katikati ya Magogoni na Kigamboni na kuzikwa jioni ya siku hiyo hiyo.

Marehemu ameacha mjane na watoto watatu, Mohammed, Said na Hosam.

0 Responses to “JK AHANI MSIBA WA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TAA, MHANDISI SULEIMANI SAID SULEIMAN”

Post a Comment

More to Read