Tuesday, January 26, 2016
KAMPUNI YA UDA YAKANUSHA KUFILISIKA
Do you like this story?
Kumekuwepo na
taarifa za uwongo kwenye vyombo vya habari, hasa kijarida cha Dira ya
Mtanzania, na mitandao ya kijamii kuhusu uongo kuwa kufilisika kwa Shirika la
Usafiri Dar Es Salaam (UDA) Limited.
Menejimenti ya
Shirika la Usafiri Dar Es Salaam inakanusha uwongo huo kuwa UDA haijafilisika
na haina dalili zozote za kufilisika isipokuwa ni Shirika namba moja
nchini na Afrika Mashariki na Kati linalokua kwa kasi ya ajabu kimaendeleo na
kibiashara.
Zifuatazo ni
takwimu zinazodhihirisha ukweli huu:
1.
UDA imeongeza idadi ya mabasi kutoka
mabasi 7 makukuu na mabovu Mwaka 2012 na kufikia takribani mabasi 400 mwaka
2015 yakiwemo mabasi 255 ya kawaida na mabasi makubwa – Hercalus, mapya na ya
kisasa kabisa duniani (ya BRT) 140.
2.
3.
Ndani ya miaka 3, kampuni ya UDA
imekuwa kwa zaidi ya asilimia 5,000
4.
Kampuni hii imeweza kufanya
maandalizi yote ya kuwezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART
Project) kwa ufanisi mkubwa. Mbali na kununua mabasi, kampuni imeweze kununua
mtambo bora na wa kisasa kabisa duniani wa kukusanya nauli na kuongezea mabasi
(Intelligent Transportation System – ITS) wenye thamani kubwa kutoka Ubelgiji
na Ujerumani. Vile vile kampuni imeweza kusaili na kufundisha madereva wa
Kitanzania zaidi ya 300 na kuwaajiri kwa ajiri ya kuendesha mradi wa mabasi
yaendayo haraka (DART Project)
5.
Kampuni imejenga karakana bora na
imara na kununua vitendea kazi vya kisasa kwa ajiri ya mabasi yake ya kawaida
na mwendo haraka.
6.
7.
Kampuni imepeleka watendaji wake
kwenye miradi mbalimbali ya BRT duniani ili kupata uzoefu wa kuwawezesha
kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi. Vile vile
Kampuni imeweza kuajiri wataalam kutoka nje (expatriates) kwa ajiri kuongezea
nguvu wataalam wake wa ndani.
Kwa takwimu
chache hizo hapo juu, Kampuni ya UDA ni namba moja Afrika kwenye sekta ya
usafirishaji wa abiria barabarani kwa idadi ya watu inaosafirisha, idadi ya
mabasi na ubora wa menejimenti.
Mafanikio haya
ya Kampuni ya UDA yanatokana na umahiri wa uendeshaji kutoka Simon Group chini
Uongozi thabiti wa Mwenyekiti wake Ndugu Robert Simon Kisena na si vinginevyo,
kama washindani wetu wavyojaribu kutuchafua kwamba kuna wanasiasa nyuma yake.
Tunawataka
washindani wetu waache tabia ya fisi ya kumfuata mtu anayetembea kwa haraka
wakidhani atandondosha mkono wapate kitoweo vinginevyo watakufa njaa.
Imetolewa
na Uongozi wa SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA) LIMITED
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KAMPUNI YA UDA YAKANUSHA KUFILISIKA ”
Post a Comment