Sunday, January 24, 2016
KLOPP AVUNJA MIWANI AKISHANGILIA USHINDI WA LIVERPOOL
Do you like this story?
Klopp akishangilia ushindi na wachezaji wake na kuvunja Miwani yake |
Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool jana
alijikuta akiharibu miwani yake mara baada ya kujumuika pamoja na wachezaji
wake kushangilia goli la ushindi katika dakika za mwisho za mchezo wao dhidi ya
Norwich uliomalizika kwa ushindi wa magoli 5-4.
Adam Lalana alifanikiwa kuwa shujaa wa mchezo
mara baada ya kufunga kwa shuti kali dakika ya 95 ya mchezo dakika chache kabla
ya Sebastian Bassong kuisawazishia Norwich na matokeo kuwa goli 4-4.
Kocha
Jurgen Klopp anasema ni mara ya pili sasa anaharibu miwani yake kwani
anakumbuka Nuri Sahin wakiwa Borussia Dortmund alimrukia wakishangilia ushindi
dhidi ya Bayern Munich, na jana ikawa ni Adam Lalana.
Lakini
pamoja na ushindi huo, kocha huyo mjerumani Jurgen Klopp 48, hakufurahishwa na
performance ya timu yake kutokana na kuruhusu mabao mengi mepesi katika michezo
yake minne mfululizo wakiruhusu bao 10 langoni mwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KLOPP AVUNJA MIWANI AKISHANGILIA USHINDI WA LIVERPOOL”
Post a Comment