Sunday, January 24, 2016

SAUTHAMPTON, HII NDIYO KAULI MPYA YA VAN GAAL KWA MASHABIKI




Boss wa Manchester United Louis van Gaal amesema yeye pamoja na kikosi chake wanastahili kuzomewa na mashabiki baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Southampton wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Old Trafford.

United imeshindwa kufunga goli kwenye dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenye mechi 11 ilizocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani kabla ya jana Charlie Austin kupachika bao la ushindi dakika ya 87.

Man United ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu England pointi tano nyuma ya Tottenham ambao wako nafasi ya nne na pointi 10 nyuma ya vinara wa ligi hiyo timu ya Leicester City.

“Wako sahihi kutuzomea. Siwezi kupinga hilo, niiliuona mchezo”, alisema Van Gaal.
“Kwa mabaya au mazuri bado tunatakiwa kuwa pamoja”, aliongeza mdachi huyo baada ya kikosi chake kupokea kipigo cha sita kwenye msimu huu.

United imefanikiwa kuvuna pointi 37 kwenye michezo yake 23, pointi chache katika historia ya klabu hiyo kwenye ligi ya England ambazo ni pointi tatu nyuma ukilinganisha na kipindi wakati yupo David Moyes msimu wa 2013-2014.
“Tunapambana japo tuna idadi kubwa ya majeruhi”, aliongeza Van Gaal.

Kwenye mchezo wa Jumamosi United ilicheza bila ya Ashley Young ambaye Van Gaal anasema anakabiliwa na majeruhi ya muda mrefu.  Pia alimpoteza mlinzi wake Matteo Darmian ambaye alitolewa uwanjani na kupelekwa moja kwa moja hospitali.

Kama beki huyo atakuwa nje ya kikosi, hiyo inamaanisha kikosi cha United kitakuwa hakina beki mzoefu wa pembeni ambaye yuko fit huku Luke Shaw akiwa bado anauguza mguu wake uliovunjika September mwaka jana.

0 Responses to “SAUTHAMPTON, HII NDIYO KAULI MPYA YA VAN GAAL KWA MASHABIKI”

Post a Comment

More to Read