Thursday, January 28, 2016

MANCHESTER CITY YATINGA FAINALI YA LEAGUE CUP, KUPAMBANA NA LIVERPOOL





Klabu ya Manchester City imefanikiwa kufuzu fainali ya Kombe la League Cup baada ya kuifunga Everton goli 3 kwa 1 katika mchezo wa nusu fainali ya pili uliochezwa katika uwanja wa Etihad unaotumiwa na Manchester City kwa michezo ya nyumbani.

Everton ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa Ross Barkley katika dakika ya 18 na baadae Manchester City kusawazisha goli dakika ya 24 kupitia kwa Fernandinho, goli la pili akafunga Kevin De Bruyne dakika ya 70 na baadae Sergio Kun Aguero kuhitimisha orodha ya magoli katika dakika ya 76.

Baada ya ushindi huo ulingano wa magoli kati ya Manchester City na Everton kuwa ni 4 kwa 3 baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa Goodison Park, Everton kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa 1 na hivyo ushindi wa goli 3 kwa 1 umeipa Man City nafasi ya kucheza fainali, Februari, 28 katika uwanja wa Wembley.

Timu nyingine ambayo imefuzu fainali ni Liverpool ambayo ilifanikiwa kufuzu hatua hiyo baada ya kuifunga kwa penati 6 kwa 5 klabu ya Stoke City ambayo katika michezo ya awali walitoka sare ya goli 1 kwa 1.

0 Responses to “MANCHESTER CITY YATINGA FAINALI YA LEAGUE CUP, KUPAMBANA NA LIVERPOOL”

Post a Comment

More to Read