Thursday, January 28, 2016
WABUNGE WA UPINZANI WATOKA TENA BUNGENI LEO
Do you like this story?
Hali ya
sintofahamu imeendelea kugubika vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma
baada ya wabunge wote wa upinzani leo kutoka nje ya bunge mara baada ya wabunge
kuanza kuchangia hotuba ya rais.
Baada ya
kipindi cha maswali na majibu, yalifuata matangazo na baada ya hapo wabunge
walitakiwa kuanza kuchangia hotuba ya Rais Magufuli lakini baadhi ya wabunge wa
upinzani walianza kuomba mwongozo kuhusu kauli ya waziri mkuu kuhusu ishu ya
michango ya chakula wanayoendelea kulipishwa wazazi wa wanafunzi wanaosoma
shule za bweni.
Hata
hivyo, licha ya baadhi ya wabunge wa Ukawa akiwemo Mbunge wa Ubungo (Chadema),
Saed Kubenea kuendelea kuomba mwongozo, naibu spika aliwanyima nafasi hiyo,
jambo lililosababisha wasusie kikao hicho na kutoka nje huku wakilalamika
kwamba wamezibwa midomo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WABUNGE WA UPINZANI WATOKA TENA BUNGENI LEO”
Post a Comment