Thursday, January 7, 2016

MREMA ASIMAMISHWA KAZI KWA URASIMU





AMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
Coat_of_arms_of_Tanzania.svg
Anuani ya Simu: “TAMISEMI”
Simu Na: (026) 2322848, 2321607
2322853, 2322420
Nukushi: (026) 2322116, 2322146
2321013
Barua pepe: ps@poralg.go.tz
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S.L.P. 1923,
DODOMA.
TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Mb) amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw. Dennis. N. Mrema kuanzia leo tarehe 07 Januari, 2016 kwa kosa la kusababisha upotevu wa Mapato ya Serikali kutokana na urasimu wa kukusudia, mazingira ya rushwa na uzembe katika utoaji wa leseni za Biashara.

Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ameelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala na nafasi yake kukaimiwa na mtu mwingine ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake.

Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI amefikia uamuzi huu baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa Wafanyabiashara ambao wamemlalamikia Mtendaji huyu kwa ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za utoaji wa Leseni za Biashara, Urasimu na Mazingira ya rushwa.

Katika uchunguzi wa awali uliofanyika kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mambo yafuatayo yamegundulika:
(i) Ukiukwajiwa Makusudi wa Sheria,  Kanuni  na Taratibu  za utoaji wa Leseni za Biashara.

(ii) Kutoa Leseni za Biashara zaidi ya 843 bila kuwa na Vyeti vya uthibitisho wa Walipa kodi ‘Tax Clearance Certificates” hivyo kuikosesha Serikali Kodi ya Mapato.

(iii) Kukaa na fomu za Wafanyabiashara 336 kwa muda mrefu bila sababu za msingi.
(iv) Kukiuka Mwongozo wa Mkataba wa Huduma kwa wateja ambao unamtaka Afisa Biashara kutoa Leseni za Biashara ndani ya siku 2 hadi 3 baada ya muombaji kuwasilisha maombi yake ya kupatiwa Leseni ya Biashara.

Aidha, Mheshimiwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais-TAMISEMI amewaagiza Maafisa Biashara wote nchini watoe huduma za Leseni kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu , kuacha urasimu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini
Ofisi ya Rais-TAMISEMI,

0 Responses to “ MREMA ASIMAMISHWA KAZI KWA URASIMU ”

Post a Comment

More to Read