Tuesday, January 5, 2016
MWIGULU AWATIMUA WALIOKULA BIL5.7 UJENZI WA MACHINJIO- RUVU
Do you like this story?
Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu. |
Mwigulu Nchemba akidadisi utunzaji wa maji ya Mifugo inayopatikana ndani ya ranchi ya Ruvu. |
Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani wakisikiliza kwa makini sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa.Anayetoa maelezo wa mwisho kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd. Bwire. |
WAKATI Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa
pongezi zao kwa serikali ya Rais. J.P.Magufuli kwa speed yake ya kuchapa
kazi, Mawaziri wake pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria
kusimamia shughuli za maendeleo ya Nchi yetu.
Hii leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye
dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi amefanya ziara ya siku moja
kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa majengo ya machinjio ya
kisasa ulioanza mwaka 2010.
Katika hali ya kusikitisha na kulazimu
kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu Nchemba amekutana na ubadhilifu wa
Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo, Fedha hizo
zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa
hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.
Waziri huyo wa kilimo amekuta mradi huo
umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila kuendelezwa, Sababu za kutelekezwa kwa
mradi huo zikidaiwa kuwa ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO
(kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu
Nchemba ambaye baada ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa
viongozi wa ranchi hiyo aliamua ifuatavyo.
Kwanza, Mwigulu Nchemba amewatimua
wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya kusimamia ranchi za
Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi
hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi
mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo la ranchi ya ruvu.
Pili, Mwigulu Nchemba amesitisha
utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa kushindwa kuchukua
hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake.
Pia, waziri huyo wa kilimo ameagiza
kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote walioshiriki ama kwa makusudi au
kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka
iwezekanavyo.
Mwisho, Nchemba amewaagiza wataalam wa
wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7 wanampelekea ripoti ya thamani ya
jengo lililokwisha kujengwa na fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa
jengo hilo.
Sambamba na hatua hizo, Mwigulu ametoa
rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi
na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya nchi yetu, Mbali na hapo, serikali
ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa
wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.
Picha/maelezo na Festo Sanga Jr.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MWIGULU AWATIMUA WALIOKULA BIL5.7 UJENZI WA MACHINJIO- RUVU”
Post a Comment