Tuesday, January 5, 2016
TUZO ZA MCHEZAJI BORA AFRIKA ...SAMATTA KUKWEA PIPA KESHO KWENDA NIGERIA
Do you like this story?
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine kesho
Jumatano anatarajiwa kuongozana na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na
klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta kuelekea nchini Nigeria kwenye
sherehe za utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora barania Afrika.
Mwesigwa
anatarajiwa kuondoka na Samatta kuelekea Nigeria katika mji wa Abuja ambapo
sherehe za utoaji tuzo hizo zitafayika Alhamisi Januari 7, ambapo siku ya
sherehe hizo Katibu Mkuu ataambatana na Ofisa ubalozi wa Tanzania nchini
Nigeria
Mbwana Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora
wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, huku pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya
Ligi ya Mabingwa (CAF CL) baada ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao 8
na kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amemtakia kila la kheri Mbwana Samatta katika
kinyanganyiro hicho cha uchezaji bora na kusema kwa niaba ya watanzania wote
wanamuombea dua njema aweze kuibuka mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa
ndani.
Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa
Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na
mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ TUZO ZA MCHEZAJI BORA AFRIKA ...SAMATTA KUKWEA PIPA KESHO KWENDA NIGERIA ”
Post a Comment