Tuesday, January 5, 2016
LWAKATARE ATEULIWA KUWA KAIMU MTENDAJI MKUU MABASI YA DRT
Do you like this story?
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene. |
TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) kwa
Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 2(2) cha Amri ya kuanzisha Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka (DART), (The Executive Agencies) (The Dar Rapid Transit
Agency) (Establishment) Order ) Tangazo la Serikali namba 120 la 2007, amemteua
Mhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo
Haraka Dar es salaam (DART) kuanzia tarehe 04/01/2016.
Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi
kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria L. Mlambo tarehe
23/12/2015. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Ronald Lwakatare alikuwa Naibu
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) akishughulikia
Ufuatiliaji na Tathmini. Mhandisi Lwakatare anatakiwa kuripoti na kuanza kazi
mara moja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Januari 05, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ LWAKATARE ATEULIWA KUWA KAIMU MTENDAJI MKUU MABASI YA DRT”
Post a Comment