Tuesday, January 26, 2016
RAIS MAGUFULI AMPONGEZA JAKAYA KIKWETE KWA KUTEULIWA NAFASI YA UMOJA WA MATAIFA KAMA MSHAURI
Do you like this story?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Mheshimiwa Ban Ki-moon kuunda jopo la watu mashuhuri watakaomshauri juu ya
namna bora ya kuendeleza na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu hususani
katika afya ya uzazi ya Mama na mtoto.
Jopo hilo la watu mashuhuri linaongozwa na wenyeviti wenza ambao ni Rais wa Chile Mheshimiwa Michelle Bachelet na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Hailemariam Desalegn, huku Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Finland Mheshimiwa Tarja Halonen wakiteuliwa kuwa wenyeviti mbadala.
Katika Pongezi hizo Rais Magufuli amesema kuteuliwa kwa Rais Kikwete kuwa miongoni mwa jopo la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumeijengea heshima Tanzania na kumechochea matumaini ya mafanikio ya kukabiliana na changamoto za afya ya mama na mtoto hususani kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Rais Magufuli ameahidi kuwa serikali yake ya awamu ya tano itatoa ushirikiano katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ambayo jopo hilo litamshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ikiwemo katika kuimarisha afya ya uzazi wa mama na mtoto.

Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
25
Januari, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ RAIS MAGUFULI AMPONGEZA JAKAYA KIKWETE KWA KUTEULIWA NAFASI YA UMOJA WA MATAIFA KAMA MSHAURI”
Post a Comment