Tuesday, January 26, 2016

UCHAGUZI WA MBUNGE WA JIMBO LA KIJITOUPELE, ZANZIBAR KUFANYIKA MACHI 20




Top of Form
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania  kuwa Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar utafanyika  mnamo tarehe 20 Machi, 2016.

Uchaguzi wa Mbunge katika Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar ni mojawapo ya Majimbo yaliyoahirisha kufanya Uchaguzi tarehe 25 Oktoba, 2015 kutokana na hitilafu kwenye Karatasi za Kura.

Aidha, Tume inapenda kuwataarifu Wananchi kuwa Watendaji (Msimamizi  wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi) walioteuliwa kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ndio watakaosimamia na kufanya shughuli za Uchaguzi  huo. Uchaguzi huo wa Ubunge katika Jimbo la Kijitoupele hautakuwa na  kampeni na Wagombea walioteuliwa kushiriki Uchaguzi ulioahirishwa mwezi  Oktoba, 2015 ndio watakaoshiriki Uchaguzi huu.

Vituo vilivyotumika katika Uchaguzi wa mwaka 2015 ndiyo  vitakavyotumika. Vituo vitafunguliwa saa 1.00 asubuhi na kufungwa saa 10.00  jioni. Watakaoruhusiwa Kupiga Kura tarehe 20/3/2016 ni wale ambao  wameandikishwa na majina yao yapo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la  Kituo na waje na Kadi ya Mpiga Kura.

Imetolewa na,
Jaji (Mst.) Damian Z. Lubuva
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
MWENYEKITI
26/01/2016
Bottom of Form

0 Responses to “UCHAGUZI WA MBUNGE WA JIMBO LA KIJITOUPELE, ZANZIBAR KUFANYIKA MACHI 20”

Post a Comment

More to Read