Tuesday, January 26, 2016
RAIS MSTAAFU DK JAKAYA KIKWETE AKABIDHI RIPOTI YA JOPO LAKE KWA BAN KI MOON
Do you like this story?
Na
Mwandishi Maalum, New York
Mwenyekiti
wa Jopo la Ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya, Rais
Mstaafu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, jana Jumatatu, amemkabidhi Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa Ban ki Moon, Ripoti ya Jopo lake.
Mhe. Jakaya
Kikwete aliteuliwa na Ban Ki Moon, kuongoza Jopo lililokuwa na wajumbe watano
mwezi Aprili 2015. kwa mujibu wa hadidu za rejea Jopo hili lilitakiwa
kutekeleza majukumu yake kuanzia mwezi Mei hadi Desemba 2015.
Akipokea
ripoti hiyo, katika hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa . Ban Ki Moon, pamoja na kumshukuru Mwenyekiti wa Jopo Mhe. Jakaya
Kikwete pamoja na timu yake, amesisitiza kwamba, mapendezo yaliyotolewa na Jopo
hilo yatazingatiwa na kufanyiwa kazi.
“ Ninatoa shukrani zangu za pekee na za dhati kwako wewe kama Mwenyekiti kwa uongozi wako , na pia kuwashukuru wajumbe uliofanya nao kazi. Ripoti hii ambayo imesheheni mapendekezo na ushauri itazingatiwa na kufanyiwa kazi”. Amesema Ban Ki Moon
Akabanisha
kwamba, mapendekeo na ushauri uliomo ndani ya Ripoti ya Jopo atauwasilisha pia
kwa Shirika la Afya Duniani ( WHO).
Katibu
Mkuu pia amesema Ripoti hiyo itasaidia sana katika kutoa mwongozo kwa Jumuiya
ya Kimataifa juu ya namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu ya afya ili
iweze kukabiliana na magonjwa ya milipuko.
Vile
vile Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemhakikishia Mwenyekiti wa Jopo Mhe.
Jakaya Kikwete na wajumbe wake kwamba, Ripoti hiyo itawekwa hadharani mapema
iwezekanavyo ili Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na makundi mbalimbali ya
jamii waweze kuisoma.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Jopo, Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
amemshukuru Katibu Mkuu Ban Ki Moon, kwa kumpatia heshima ya kuongoza Jopo
hilo, jopo ambalo amesema walifanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu.
Wajumbe
wengine wa Jopo hilo walikuwa ni Bw. Celso Amorim ( Brazil), Micheline Calmy (
Switzerland), Marty Natalegawa ( Indonesia) Joy Phumapi ( Botswana) na Rajav
Shah ( USA).
Jukumu
kubwa ya jopo hilo kwa mujibu wa hadidu za rejea, pamoja na mambo mengine,
lilikuwa ni kutoa mapendekezo ya namna ya kuimarisha mifumo ya kitaifa na
kimataifa katika kuzuia na kukabiliana na majanga ya kiafya yakiwamo magonjwa
ya mlipuko, ikiwa ni pamoja na kujifunza kuhusu mwitikio wa Jumuiya ya Kimataifa
kufuatia kuibuka kwa janga la ugonjwa wa Ebola.
Katika
utekelezaji wa majukumu yake Jopo lilikutana na kufanya majadiliano ya kina na
makundi mbalimbali yakiwamo ya wataalamu, wawakilishi wa nchi tatu ambazo
ziliathirika sana na ugonjwa wa Ebola ( Liberia, Siera Leone na
Guinea),Mashirika ya Kimataifa na Kikanda , Taasisi za Fedha za kimataifa,
wahudumu wa Afya, Wasomi , Watafiti, Sekta Binafsi na wataalam wa fani na kada
mbalimbali.
Top of Form
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ RAIS MSTAAFU DK JAKAYA KIKWETE AKABIDHI RIPOTI YA JOPO LAKE KWA BAN KI MOON”
Post a Comment