Tuesday, January 26, 2016
WASICHANA BIKIRA KUSOMESHWA BURE.!!
Do you like this story?
Mashirika
ya kutetea haki za binaadamu nchini Afrika Kusini, yanasema yamekasirishwa na
mpango wa
kuwapa
ufadhili wa elimu ya vyuo vikuu wasichana 16 ikiwa watabakia bikira.
Wasichana kutoka wilaya ya Uthukela ya mkoa wa mashariki wa
KwaZulu-Natal, wana fursa ya kupewa msaada wa elimu wa hadi miaka mitatu, ili
kugharamia masomo yao katika chuo kikuu.
Meya wa eneo hilo Jabulani Mkhonza amesema kuwa, wasichana
wanaishi katika hatari kubwa ya kunyanyaswa, kupata mimba na hata kuambukizwa
virusi hatari vya Ukimwi.
Lakini wapinzani wanasema mpango huo ni wa kuwadunisha
wanawake, wakiongeza kuwa pesa za walipakodi hazipaswi kutumiwa kukiuka haki za
wasichana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WASICHANA BIKIRA KUSOMESHWA BURE.!! ”
Post a Comment