Tuesday, January 26, 2016
TRA YAWAOMBA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO
Do you like this story?
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa
kutoa taarifa za Maafisa wanaofanya kazi kinyume na maadili.
Akiongea na mwandishi wa habari hii leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA), Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina
Idara Maalumu ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo
inashughulika na kufuatilia maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.
“Tunawaomba wananchi kushirikiana na Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa
kuwapa taarifa juu ya maafisa wa TRA wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi
wa Umma,”alisema Kayombo.
Mkurugenzi Kayombo ameongeza kuwa wananchi wanaweza kutoa taarifa kwa
kupiga simu kwa namba 0689122515 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwa simu namba
0689122516 na kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu
husika na zitafanyiwa kazi.
Aidha Kayombo amependa kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa namba hizo ni za
siri na hakuna mwananchi atakayepata tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maafisa
wasio na maadili.
TRA kupitia Idara yake ya Mambo ya Ndani imepokea malalamiko mengi kutoka
kwa wananchi juu ya watumishi wa TRA wanaoenda kinyume na maadili, wameyafanyia
uchunguzi na baadhi ya watumishi wamefukuzwa na wengine kupewa adhabu kali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TRA YAWAOMBA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO ”
Post a Comment