Wednesday, January 27, 2016
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU ATANGAZA KIAMA KWA WALA RUSHWA HASA WATUMISHI WA UMMA.
Do you like this story?
Baadhi ya wakurugenzi wa Taasisi hiyo wakiwa katika mkutano huo. |
Mwendeshaji wa Mtandao wa Fullshangwe, John Bukuku (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo. |
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), imetoa onyo kwa taasisi
nyeti nne hapa nchini ikiwemo wanaohusika na matumizi ya fedha za Umma kufuata
sheria, taratibu na kanuni.
Pia,Takukuru
inashughulikia kukamilisha kesi kubwa 36, zinazowahusu watumishi wenye
ushawishi na hadhi kubwa hapa nchini ambapo kati ya hizo zipo zilizokamilika na
kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Valentino Mlowola
alisema kumekuwepo na malalamiko mengi kwa wananchi kuwajulisha matendo ya
rushwa na ufisadi yanayoendelea hapa nchini.
Alisema
kutokana na hali ya wananchi kuona nia ya serikali ya awamu ya tano katika
kushughulikia matatizo ya rushwa na ufisadi hapa nchini ametoa ovyo kwa maofisa
wa umma wanaofanya rushwa na ufisadi kuwa sehemu yao ya kazi na miradi ya
kuwaingizia kipato.
“Natoa
onyo kwa maofisa wa umma ambao wamefanya rushwa na ufisadi kuwa ni sehemu ya
kazi zao na miradi ya kuwaingizia kipato, wajitafakari kabla hawajaamua
kujihusisha na vitendo vya rushwa,”alisema.
Alisema
hawatasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumishi watakaojiingiza katika
kulihujumu taifa na wananchi kwani wananchi wanakiu ya kupata maendeleo na
maisha bora na kuwataka watambue wananchi wa jana si wa leo kwani wamedhamiria
kuunga mkono juhudi za serikali yao.
Mlowola
alitoa ovyo kwa maofisa maduhuli na watekelezaji wa jukumu la kukusanya kodi za
wananchi kwa kutomuonea mtu haya kwa atakayejihusisha na ubadirifu wa fedha na
mali ya umma.
“Wakusanye
kodi halali ya serikali kwa kufuata sheria, taratibu na Kanuni zinazowaongoza
kukusanya kodi, tutachukua hatua stahiki pale kutakapokuwa na ukiukwaji wa
sheria, taratibu na kanuni zilizopo,”alisema.
Pia,
Mlowola alitoa ovyo kwa watakaohusika kwenye matumizi ya fedha za umma kwamba
wafuate sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza kwani taasisi hiyo
haitawavumilia watakaokiuka fedha za serikali isiyo halali.
Mbali
na hilo, pia Kaimu huo alitoa onyo kwa watumishi wa umma wenye jukumu la
kuhudumia mahitaji ya umma kwa kutojihusisha na rushwa kwa kutekeleza majukumu
yao katika muda uliotakiwa, weledi na uaminifu.
Alisema
taasisi hiyo haipo kwa lengo la maslahi ya watu wabadhilifu wa mali ya umma
kwani uchunguzi wa kesi ya kuisababishia hasara serikali shilingi bilioni 8.5
kutokana na ukwepaji wa kodi wa kampuni ya Mafuta ya Lake Oil kwa kufanya
udanganyifu kuuza mafuta ndani ya nchi Petrol lita 17,461,111.58 kwa kudanganya
zilisafirishwa umefikia hatua nzuri.
“Takukuru
imekamilisha shauri la hili na mtuhumiwa wamepewa miezi miwili kurejesha
mikononi fedha zote na kuwarudisha mahakamani endapo watashindwa kurejesha
kiasi hicho,”alisema.
Alisema
mbali na shauri hilo, wapo kwenye hatua nzuri ya kukamilisha uchunguzi wa kesi
ya hati fungani ya malipo yaliyolipwa na kampuni ya Enterprise Growth Markert
Advisor(EGMA), kiasi cha dola 6,000,000 kwa lengo la kuisaidai Tanzania kupata
mkopo wa dola 600,000,000.
“Takukuru
imebaini fedha hizo dola 6,000,000 zilitakatishwa na watumishi wa umma wasio
waaminifu wakishirikiana na baadhi kutoka sekta binafsi huku wakijua fedha hizo
wamezipata kwa njia haramu,”alisema.
Akizungumzia
hatua aliyochukua rais, Dk. John Magufuli kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa
Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Mhandisi Benhadard Tito kwa tuhuma zinazomkabili
tayaari wanachunguza shirika hilo la reli.
Alisema
kulikuwepo na ukiukwaji wa kuwapata wazabuni kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya
kimataifa(Standard Gauge) unaosimamiwa na Shirika la Hodhi la Reli
Nchini(RAHCO), wanamekamatwa ikiwemo raia wa Kenya aliyekuwa kwenye mchakato
huo, Kanji Muhando.
Kaimu
huyo alisema shauri la kesi ya mabehewa ya kokoto 25 ya shirika la reili nchini
(TRL), ya kukiuka sheria ya manunuzi ya umma Na.21/2004 pamoja na kanuni zake
kutoka kampuni ya Hindustha Engineering and Industries Limited limekamilika.
“Uchunguzi
umekamilika na tumeshapeleka kwa mkurugenzi wa Mashtaka kuomba kibali cha
kuwafikisha watuhumiwa waliobainika kujihusisha na matendo ya rushwa na
ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni za ununuzi wa umma mahakamani,”alisema.
Alisema
rais alijipa kazi ya kutumbua majipu hivyo aliwasihi watumishi wa taasisi hiyo
kutumikia wananchi kwa eledi huku akibainisha tayari wanatekeleza azma na
dhamira ya rais ya kupambana na rushwa.
Akitolea
ufafanuzi swala la kumsubiri rais kutumbua majipu ndio taasisi hiyo ifanye
ufafanuzi, Mlowola alisema taasisi hiyo imejipanga vilivyo tangu Novemba 20
mwaka jana wakati rais alipohutubia bungeni alipoonesha dhamira ya na nia ya
dhati ya kupambana na rushwa na ufisadi bila kumuonea mtu haya.
“Nitoe
rai kwa wananchi kutoa taarifa ili tuweze kujua kabla hatujapigwa, tukiweza
kuisaidia serikali kuokoa fedha kabla hatujapigwa zitasaidia wananchi
kutoa elimu bure, upatikanaji wa dawa na mishahara mizuri,”alisema.
Alisema
tayari wameshaanza kuchunguza madai ya aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kwani tayari wapo hata viongozi wakubwa.
“Siwezi
kusema kuwa kulikuwa na ulegevu, na hatua zimechukuliwa nchini imefikisha
mhakamani mawaziri ila nchi ipo kwenye ufagio mpya hivyo tumeweka nguvu zaidi
na hali zaidi,”alisema.
Akizungumzia
maofisa takukuru waliofukuzwa kazi a rais baada ya kukiuka maagizo ya rais ya
kupata kibali cha kusafiri nje, alisema maofisa hao walikwenda kwenye mkutano
wa taaisis za kupambana na rushwa uliofanyika Congo-Kinshasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KAIMU MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU ATANGAZA KIAMA KWA WALA RUSHWA HASA WATUMISHI WA UMMA.”
Post a Comment