Sunday, January 17, 2016
RASMI: YANGA YAMREJESHA NIYONZIMA KUNDINI KUJIUNGA NA KIKOSI
Do you like this story?
Kiungo wa kutumainiwa wa Yanga na timu ya
taifa ya Rwanda amerejea kwenye timu yake ya Yanga baada ya kutimuliwa na
uongozi huo kutokana na sababu za kinidhamu.
Leo January 17, 2016 Niyonzima ameomba radhi
kwa wanachama, viongozi na wachezaji wenzake kwa kile ambacho kilitokea miezi
michache iliyopita. Niyonzima ameshaomba radhi mbele ya waandishi wa habari na
kwa sasa anasubiri taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa Yanga kuhusu suala
kusamehewa kwake.
“Nitumie fursa hii kuwaomba radhi viongozi,
wanachama, wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wa Yanga kutokana na
yale yote yaliyopita nyuma. Mimi niliondoka kwenda kuichezea timu yangu ya
taifa ya Rwanda lakini nilichelewa kurejea kwenye klabu yangu na hapo ndipo
matatizo yalianza”, amesema Niyonzima.
“Kiukweli nilikosea kwasababu sikutoa taarifa
kwa timu yangu na ikachukua uamuzi wa kunifukuza kwenye timu, lakini tumekaa
chini na kuzungumza na uongozi na kufikia sehemu nzuri ndiyo maana mpaka sasa
niko hapa”
“Nilistushwa na uamuzi ambao ulichukuliwa na
klabu yangu kwasababu sikutarajia kitu kama hicho kingetokea, kiukweli nilikuwa
surprised na niliumizwa na uamuzi huo lakini nashukuru mambo haya yamefikia
hatua nzuri”.
Msemaji wa Yanga Jerry Muro amesema uongozi
wa klabu yake unajipanga kutoa taarifa rasmi kuhusu suala la Niyonzima ambayo
itahitimisha mjadala kuhusu kiungo huyo.
“Sisi kama uongozi wa Yanga, tunamshukuru
Niyonzima kwa kuwa muungwana juu ya hili suala na kuamua kuja kwa uongozi wa
Yanga na kuomba radhi kwa yote yaliyotokea”, amesema Muro.
“Niyonzima kwetu ni kama mtoto kwa hiyo
uongozi umekaa na kuzungumza naye na utatoa taarifa rasmi hivi karibuni na
kuhitimisha mjadala wa mchezaji huyo”.
Haruna Niyonzima alifungashiwa virago na
uongozi wa Yanga kutokana na sababu za utovu wa nidhamu ambao umekuwa
ukijirudia kila mara hasa kuchelewa kurudi pindi anapokweda nyumbani kwao
kuitumikia timu yake ya taifa au anapokuwa kwenye mapumziko ya likizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RASMI: YANGA YAMREJESHA NIYONZIMA KUNDINI KUJIUNGA NA KIKOSI”
Post a Comment