Wednesday, January 27, 2016

SIMBA ITACHUKUA UBINGWA WA VPL? HAYA NDIYO MAJIBU YA HAJI MANARA




Baada ya kikosi cha Simba kumaliza raundi ya kwanza kikiwa nyuma ya vinara wa ligi kwa pointi sita, bado wanauota ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kutua kwa kocha Jackson Mayanja ambaye kwa sasa anakinoa kikosi hicho baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr.

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema, mikakati iliyopo sasa ni kuhakikisha Simba inapata matokeo mazuri ambayo wanauhakika yataendelea kuwafanya wapambane na wapinzani wao kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

“Tunaingia katika raundi ya lala salama tukiwa na mtazamo positive kwamba tunazo chances za kuchukua ubingwa, kwa hesabu zilivyo, tumezidiwa pointi sita na wapinzani wetu. Pointi sita ni maana ya michezo miwili, kuna michezo 15 inakuja ya ligi kuu. Kwahiyo uongozi mzima wa klabu ya Simba, benchi la ufundi na wachezaji focus yao ni kuchukua ubingwa”, amesema Manara.

“Tunajua ligi ni ngumu hakuna mechi nyepesi lakini tunaamini bado tunao uwezo mkubwa wa kuchukua ubingwa kutokana na maboresho ambayo yamefanywa katika kikosi cha Simba hususan katika benchi la ufundi baada ya kuingia mwalimu Jackson Mayanja, tunaona kuna kitu kinakuja kile ambacho mashabiki wa Simba wanaona tunakikosa”.

Raundi ya kwanza imemalizika huku kikosi cha Simba kikiwa kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kikiwa na pointi 33 nyuma ya Yanga na Azam zenye pointi 39 lakini Yanga inakaa kileleni kutokana na tofauti ya magoli dhidi ya Azam.

0 Responses to “SIMBA ITACHUKUA UBINGWA WA VPL? HAYA NDIYO MAJIBU YA HAJI MANARA”

Post a Comment

More to Read