Monday, January 18, 2016

UMEIPATA HII: MTU MWENYE VIDOLE VINGI DUNIANI





Na Gabriel Ng’osha na Mtandao
Ni vigumu kuamini! Raia wa Himatnaga, Gujarat nchini India, Devendra Suthar amebainika kuwa ndiye mtu aliye hai mwenye vidole vingi zaidi vya mikononi na miguuni. Devendra ambaye ni fundi seremala ana vidole 14 vya mikono na 14 vya miguuni hivyo jumla kuwa na vidole 28 hivyo kuweka rekodi katika Kitabu cha Kumbukumbu cha Dunia cha Guinness.

Ingawa katika shughuli zake za useremala vidole hivyo havimsumbui wala kumkwamisha katika ufanyaji wa kazi, lakini huwa makini sana katika shughuli za ukataji wa vitu mbalimbali.

0 Responses to “ UMEIPATA HII: MTU MWENYE VIDOLE VINGI DUNIANI ”

Post a Comment

More to Read