Saturday, January 23, 2016
UMEYA JIJI LA DAR WAPIGWA KALENDA
Do you like this story?
Mkuu wa Kitengo cha Itifaki na Uhusiano na Umma wa Jiji, Gaston Makwembe (kushoto) |
HALMASHAURI ya
jiji la Dar es Salaam imeahirisha uchaguzi wa meya wa Jiji uliokuwa ufanyike
leo, mpaka hapo tarehe itakapotangazwa baadaye.
Mkuu wa Kitengo
cha Itifaki na Uhusiano na Umma wa Jiji, Gaston Makwembe alisema uchaguzi huo
uliokuwa ufanyike leo saa nne asubuhi katika ukumbi wa Mmikutano wa Karimjee,
umeahirishwa.
Alisema tarehe
ya uchaguzi huo itapangwa baadaye na taarifa zitatolewa kwa wananchi kupitia
vyombo vya habari bila kueleza sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Uchaguzi huo
unatarajiwa kuwa na mvutano wa aina yake kati ya vyama vinavyounda na Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika uchaguzi
huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM ) kinawakilishwa na Diwani wa Kinondoni, Yusuph
Omary Yenga, Ukawa kwa mwamvuli wa Chadema wanawakilishwa na Diwani wa Kata ya
Vijibweni, Isaya Mwita, huku mgombea wa nafasi ya Naibu Meya akitarajiwa kutoka
CUF.
Awali, Ofisa
Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alitoa wito kwa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kusimamia uchaguzi huo kwa amani na haki
ili usifanyike kama wa kumtafuta meya wa Ilala na Kinondoni uliokuwa na
mizengwe mingi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UMEYA JIJI LA DAR WAPIGWA KALENDA ”
Post a Comment