Thursday, January 7, 2016

WAKATI KENYA, UGANDA, BURUNDI NA RWANDA ZIMETOA WAAMUZI WA KUCHEZESHA CHAN, UNAJUA BONGO WAMETOKA WANGAPI?




Majina ya waamuzi pamoja na waamuzi wasaidizi yameshatangazwa kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani CHAN michuano ambayo itafanyika mwaka huu nchini Rwanda.

Waamuzi 34 kutoka mataifa 24 wamechaguliwa kwa ajili ya kupuliza firimbi na kushika vibendera wakati wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza rasmi January 16 hadi February 7, 2016 ili kukakikisha kila kitu kinakwenda sawa wakati wa michuano hiyo ambayo timu ya taifa ya Tanzania ilishindwa kufuzu baada ya kulambishwa mchanga na wababe Uganda.

Kitu cha kushangaza kuliko vyote ni kukosekana kwa jina hata moja la mwamuzi kutoka Tanzania hata kwenye orodha ya waamuzi wasaidizi. Majina ya waamuzi na waamuzi wasaidizi watakaochezesha michuano hiyo yanatoka kwenye mataifa mengine ya Afrika huku nchi za Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda wakitoa waamuzi kwa upande wa ukanda wa Afrika Mashariki lakini Tanzania hoi.

Wakati Tanzania tunajifariji soka letu linakua, tuna professional ligi lakini nadhani wanaotutazama ndio wanajua kiwango cha soka letu ndiyo maana hakuna hata mwamuzi mmoja kutoka Bongo atakayeshezesha michuano hiyo.
Timu yetu ya taifa ilishindwa kufuzu kucheza michuano hiyo kwasababu tulizidiwa uwezo na wapinzani, lakini na hili la waamuzi limekaaje?

Waamuzi ambao wanachezesha mechi za ligi kwa kukopwa, wanatengenezewa mazingira ya kuuza mechi kutokana na njaa waliyonayo hawawezi kuwa na vigezo vya kuchezesha michuano mikubwa kama hii kwasababu watawaharibia watu mashindano.

Sisi tubaki tu na ligi yetu ya kiujanja-ujanja na mashindano yetu ya Mapinduzi Cup ambayo ‘marefa’ wanakataa magoli halali kwa kutokujua sheria  barabara. Ifike mahali Tanzania tukubali tu kuanza upya lakini tusilazimishe au kujifariji sisi ni wa hadhi flani wakati ukweli tunaujua wenyewe.

Hii ni orodha ya waamuzi watakaochezesha michuano ya CHAN 2016 nchi Rwanda:
REFEREES

#
NAMES
COUNTRY

1
Abid Charef Medhi
Algeria

2
Bernard Camille
Seychelles

3
Denis Dembele
Cote d’Ivoire

4
Ibrahim Nour El Din
Egypt

5
Daniel Bennet
South Africa

6
Kordi Med Said
Tunisia

7
Mohamed H. El Fadil
Sudan

8
Nampiandraza Hamada
Madagascar

9
Keita Mahamadou
Mali

10
Ali Lemghaifry
Mauritania

11
Malang Diedhiou
Senegal

12
Zio Ephrem Juste
Burkina Faso

13
Davies Omweno
Kenya

14
Hudu Munyemana
Rwanda

15
Joseph Lamptey
Ghana

16
Thierry Nkurunziza
Burundi


Orodha ya waamuzi wasaidizi wa michuano ya CHAN 2016-Rwanda
ASSISTANT REFEREES

1
Mokrane Gourari
Algeria

2
Ndagijimana Theogene
Rwanda

3
Mark Ssonko
Uganda

4
Oamogestse Godisamang
Botswana

5
Noupue Nouegoue Elvis
Cameroon

6
Dina Bienvenu
Benin

7
Serigne Cheikh Toure
Senegal

8
Ahmed Hossam Taha
Egypt

9
Tesfagiorghis Berhe
Eritrea

10
David Laryea
Ghana

11
Mamady Tere
Guinea

12
Sullaymane Sosseh
Gambia

13
Marwa Range
Kenya

14
Mahamadou Yahaya
Niger

15
Hensley Petrousse
Seychelles

16
Khumalo M. Steven
South Africa

17
Theophile Vinga
Gabon

18
Nabina Blaise Sebutu
DR Congo


0 Responses to “WAKATI KENYA, UGANDA, BURUNDI NA RWANDA ZIMETOA WAAMUZI WA KUCHEZESHA CHAN, UNAJUA BONGO WAMETOKA WANGAPI?”

Post a Comment

More to Read