Thursday, February 25, 2016
BENKI YA NMB YAZINDUA PROMOSHENI YA PATA PATIA.
Do you like this story?
Benki ya NMB imezindua mchezo wa bahati
nasibu kwa wateja wake ambapo watakuwa na nafasi ya kujishindia kuanzia
shilingi 100,000/- hadi shilingi milioni tatu 3,000,000/-. Bahati nasibu hiyo
imepewa jina la “Pata Patia” ambapo jumla ya shilingi milioni 300 zitashindaniwa.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, Kaimu Mkuu wa Kitego cha Wateja Binafsi Boma Raballa alisema kwamba
Promosheni ya Weka Ushinde na NMB’ itakuwa na washindi kila wiki na kila mwezi
na ni ya kipekee ya wateja wa zamani na wapya
Bw. Raballa aliongeza kuwa ” Wateja
watatakiwa kuweka fedha katika akaunti yoyote ya NMB kiasi cha chini kikiwa ni
Shilingi elfu hamsini (50, 000) ili kupata nafasi ya kushinda na zaidi uwekavyo
fedha utapata nafasi zaidi ya kushinda. Wateja wanaweza kuweka fedha kupitia
tawi letu lolote, NMB Wakala na NMB mobile.”
Promosheni hii itakuwa na droo za kila mwezi
ambapo tawi husika la benki ya NMB litawasiliana na washindi 24 kila mwezi
kuzungusha gurudumu la bahati katika matawi yaliyochaguliwa na NMB.
NMB imetenga jumla ya shilingi milioni 300
kushindaniwa. Washindi 144 ambao ni wateja wa zamani na wapya wanaweza kushinda
hadi shilingi 3,000,000/= kila mmoja; jumla ya washindi 24 watabainishwa kila
mwezi kwa kipindi cha miezi sita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BENKI YA NMB YAZINDUA PROMOSHENI YA PATA PATIA.”
Post a Comment