Thursday, February 25, 2016

NAIBU SPIKA ATOA MSAADA WA MILLIONI TANO(5) SHULE ALIYOSOMA. MBEYA


NAIBU spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson Mwansasu akizungumza na wanafunzi mara Baada ya kufika Shuleni hapo.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

NAIBU spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson Mwansasu akipokelewa na Mkuu wa Shule ya wasichana Loleza Mwalimu Emily Fwambo Mara Baada ya kuwasili Shuleni hapo.
.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)




Maabara ya masomo ya sayansi


NAIBU spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson Mwansasu akilitizama Bweni Ambalo alikuwa analala.

Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philip Mulugo akizungumza na Wanafunzi.

Hili Ndio Bweni Ambalo Mh Tulia Ackson Mwansasu alikuwa anaishi kipindi anasoma.


Mkuu wa Shule ya wasichana Loleza Mwalimu Emily Fwambo akisoma Taarifa ya shule.





NAIBU spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson Mwansasu ametoa msaada wa shililingi milioni tano kwa ajili ya ukarabati wa bweni la Mapinduzi katika Sekondari  ya Loleza Mkoani Mbeya.

Amefikia hatua ya kutoa kiasi hicho kwa ajili ya ukarabati katika bweni ambalo aliishi wakati akisoma elimu ya Sekondari kati ya mwaka 1991-1994 alipo hitimu kidato cha nne,baada ya kuona halitumiki kutokana na uchakavu wa dali hali iliyo lazimu uongozi wa shule kulifunga kutokana na kuhatarisha maisha ya wanafunzi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea majengo mbalimbali ya shule hiyo Mwansasu alisema kuwa licha ya kuwa kuna changamoto nyingi katika shule lakini amesikitishwa zaidi kuona bweni ambalo aliishi ndani ya miaka minne likiwa limechakaa na halitimuki tena.

Kutokana na kujionea uchakavu huo Naibu Spika Mwansasu alisema kuwa ameamua kutoa kiasi hicho cha fedha huku akiahidi kuendelea kusaka wafadhili mbalimbali ili wawezi kusaidia kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoikabali shule hiyo kongwe hapa nchini ikiwemo ukachakavu wa miuondo mbinu ya madarasa na mabweni.

Katika hatu nyingine amewasii wanafunzi  shule hiyo kusoma kwa bidii huku wakimtumainia Mungu na kuwataka wanafunzi hao kutambua kuwa wanategemewa na familia pamoja na taifa kwa jumla hivyo wanapaswa kusoma kwa kujituma katika masomo yao ili waje kulitumikia taifa kama ambavyo yeye alijituma na hatimeye leo amepata fursa ya kulitumikia taifa.

Mbali Naibu Spika kutoa kiasi hicho  la kiasi hicho cha fedha lakini pia Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philip Mulugo ambaye aliambatana naye katika zaira hiyo  alitoa shilingi milioni moja kwa ajili ya ukarabati wa miondombinu shule hapo.

Akisoma taarifa ya shule Mkuu wa Shule hiyo Emily Fwambo alisema kuwa shule hiyo ambayo ilinzishwa mwaka 1948 ikiwa chini ya Wamishinari wa Kinglikana na baadaye mwaka 1969 kuwa chini ya Serikali imekuwa ikifanya vizuri katika mitahani ya kidato cha Sita kitaifa kwani matokeoa ya mwaka jana kidato cha sita wanafunzi walifauli kwa asilimia mia moja.

Amesema kuwa licha ya kuwa na mafanikio hayo kitaalumu lakini shule hiyo  imeikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa uzio kiasi kinacho palekea wanafunzi kuruka na kwenda kuzurula mitaani.

Aidha Mkuu wa huyo amesema mbali na uzio lakini pia shule hiyo ambayo ina kidato cha tano na sita pekee inakabiliwa changamoto ya bwalo la chakula hali inayo walamizimu wanafunzi kula chakula wakiwa wamesimama na wengine wakilazimika kukaa nje.

‘Mheshimiwa Naibu Spika kwanza nishukuru kwa ujio wako lakini pamoja mafanikio tuliyo nayo kitaaluma lakini tuna changamoto ikiwemo uhaba wa madarasa, uzio na uchakavu wa mabweni, kubwa ni hili na bwalo la chakula kwani awali lilijengwa kwa ajili ya kuhudumia wanafaunzi 300 lakini mpaka sasa tunawafunzi 831 hivyo tunahitaji msaada wako wa hali na mali ili kuondokana na changamoto hizi’ alisema Fwambo mkuu wa shule hiyo ambaye pia ni muhitimu wa kidato cha nne mwaka 1986

Aliongeza kuwa kwa upande wa mabweni shule hiyo inayo 18 lakini ni mabweni 16 ndiyo yanayo tumika na mawili hayatumiki likiwemo bweni la Mapinduzi ambalo aliishi akiwa anasoma.

Aliongeza kuwa kutokana na watalaamu kufanya upembuzi shule hiyo inahitaji mabati 393 geji 28 ili kukamilisha majengo yote.
mwisho

0 Responses to “NAIBU SPIKA ATOA MSAADA WA MILLIONI TANO(5) SHULE ALIYOSOMA. MBEYA”

Post a Comment

More to Read