Monday, February 29, 2016
IBRAHIM AJIB AKABIDHIWA TUZO YA MCHEZAJI BORA
Do you like this story?
Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group Richard Mvula Akimkabidhi mchezaji wa Simba Mshindi
wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib. |
Katika
kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba
ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.
Mshindi
wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi zaidi
zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla
kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.
Akikabidhiwa
tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na
Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group ambao ni
washauri na watekelezaji wa Masoko na
Biashara wa Simba, Richard Mvula, Ibrahim Ajib alisema “kila siku nimekuwa
nikiendelea kujitahidi kufanya vizuri zaidi ili nami ifike siku niweze
kukabidhiwa tunzo hii, kwakweli ni heshima kubwa sana kwangu, napenda kuchukua
fursa hii kuupongeza uongozi mzima wa Simba kwa kuanzisha utaratibu huu, pia
napenda kuwashukuru mahsbiki wangu ambao wamenipigia kura, wachezaji wenzangu
kwenye kikosi cha Simba ambao kila siku tumekuwa tukishirikiana katika kazi
yetu hii ya mpira, napenda kushukuru kwa sapoti kubwa ninayoipaa kutoka kwa
familia yangu na mwisho napenda kumshukuru Allah kwa kuendelea kunibariki na
neema zake kila siku”
Akimakabidhi
tunzo hiyo Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group Richard
Mvula alisema “kama mtakumbuka utaratibu huu ulianzishwa kwa ajili ya kuwapa
motisha wachezaji wetu na sasa umekuwa ni utamaduni wetu katika kuwapongeza na
kuonesha kuthamini jitihada zinazofanywa na wachezaji wetu katika kuutafuta
ushindi wa msimu huu”
Napenda
kuwakumbusha wanachama na wapenzi wa Simba kuendelea kuwapa sapoti wachezaji
wetu kwani kwa sapoti yao ndio mafanikio ya timu yetu yanapopatikana, aliongeza
Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group Richard Mvula
Akizungumza
jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group,
Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio
watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza
kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia
mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa
Simba”.
Tukumbuke
kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa umejiunganisha na huduma ya
Simba News kwa kutuma jina la mchezaji kwenda namba 15460. Zoezi la kumchagua
mchezaji bora wa mwezi wa Januari, 2016 litaanza February 29
2016. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata mchezaji wako bora wa
Mwezi Januari, 2016.
Simba
News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari
mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji
wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiunga na
Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ IBRAHIM AJIB AKABIDHIWA TUZO YA MCHEZAJI BORA”
Post a Comment